MAMLAKA HUSIKA ZATAKIWA KUONGEZA KASI KUBAINI WOTE WALIOSABABISHA KUANGUKA KWA JENGO

 
Rais JAKAYA KIKWETE amezitaka Mamlaka husika kuhakikisha zinaongeza kasi ya uchunguzi ili kuwabaini watu wote waliosababisha kuanguka kwa Jengo la Ghorofa 16, katika Mtaa wa Indira Gandhi, Jijini Dar es salaam na kusababisha vifo vya watu 34 huku wengine 18 wakijeruhiwa katika tukio hilo.
Rais KIKWETE ametoa kauli hiyo wakati wa zoezi la kutoa vyeti kwa Walioshiriki katika uokoaji mara baada ya kuanguka kwa jengo hilo, Machi 29, mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya kuwashukuru kutokana na mchango wao.
Amesema ni lazima watu watakaobainika kusababisha maafa hayo kutokana na uzembe wao wahojiwe ili ukweli ubainike.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam SAID MECK SADIKI, anafafanua zaidi kuhusina na watu wanaoshikiliwa hadi sasa kutokana na tukio hilo.
Nao baadhi ya Washiriki waliokabidhiwa vyeti hivyo akiwemo, Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, Kamishina ROGATIUS KIPALI na Mwakilishi wa Longxing International Ltd, MOHAMED MAZRUI, wanatoa rai yao kufuatia kuanguka kwa Jengo hilo.
Miongoni mwa Washiriki wa Uokoaji waliopewa vyeti hivyo kutokana na mchango wao ni pamoja na Vikosi vya Ulinzi na Usalama nchini, Mashirika ya Serikali na ya Watu binafsi, Vyombo mbalimbali vya habari nchini

Post a Comment

Previous Post Next Post