Progaramu maalumu ya TEKU ya kufanya/kurudia Mtihani wa Kitaifa wa kidato cha nne

 
Fomu ya maombi imepachikwa hapo chini, bofya maneno yaliyoandikwa “Download File” kupakua nakala.

KURUGENZI YA ELIMU ANUAI

PROGRAMU MAALUMU YA KUWAANDAA WATAHINIWA  KUFANYA/KURUDIA MTIHANI WA TAIFA KIDATO CHA  NNE-2013/2014


Chuo Kikuu Teofilo Kisanji (TEKU) kinakaribisha  maombi kutoka Kwa watahiniwa wote waliomaliza Kidato cha Nne kujiunga na program maalumu.

Lengo la programu hii maalumu ni kuwawezesha watahiniwa wanaopenda kujiunga na kidato cha Tano pamoja na kozi
mbalimbali za cheti na stashahada kupata sifa itakazowawezesha kuendelea na masomo kwangazi husika.

Masomo yataanza tarehe 30/4/2013 na yataendeshwa kwa muda wa miaka miwili tu.  Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 28 /3/ 2013 na usajili utafanyika tarehe 28/3/203.
 
Masomo yatakayofundishwa ni kama ifuatavyo: Uraia (Civics), Historia (History), Jiografia (Geography), Kiswahili, Kiingereza (English), Fizikia (Physics), Kemia (Chemistry), Biolojia (Biology), Hisabati (Basic Mathematics) na Fasihi ya Kiingereza (Literature in English)

Sifa za Mwombaji: Mwombaji awe na namba ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne

Ada kwa mwaka ni Tsh. 430,000/=
Malipo haya yanalipwa moja kwa moja  kwenye akaunti za Chuo Kikuu Teofilo Kisanji hayajumuishi gharama za malazi, chakula na usafiri.

 Akaunti za Chuo ni kama ifuatavyo:

Teofilo Kisanji University
NBC   Account no. 016103001650
STANBIC Account no. 0140015028101
CBA Account no. 0300786000
CRDB account no. 01J1065895000

Fomu zinapatikana chuoni, eneo la Kitalu  T,  Mbeya mjini na vilevile mwombaji anaweza kuzipata kutoka katika Tovuti ya chuo: www.teku.ac.tz - Appplication form for Admission to Form IV students who failed National Examinations in 2013 year.

Maombi yatumwe kwa:

Mkurugenzi,
Kurugenzi ya Elimu Anuai
Chuo Kikuu Teofilo Kisanji
Kampasi ya Zamani, Kitalu. T
S.L.P. 1104
Mbeya
TANZANIA

Simu: +2550252502682
Faksi: 2550252503721
Baruapepe: info@teku.ac.tz
Tovuti:   www.teku.ac.tz
Application Form Form IV 2012/20131.pdf
Download File

Post a Comment

Previous Post Next Post