Polisi nchini Pakistan wamemtia mbaroni rais wa zamani wa nchi hiyo Jenerali Mstaafu Pervez Musharraf.
Musharraf amekamatwa leo nyumbani kwake mjini Islamabad na kufikishwa mahakamani.
Kiongozi
huyo alirejea Pakistan mwezi uliopita, akitarajia kuwania ubunge katika
uchaguzi mkuu mwezi ujao, baada ya kuwa uhamishoni kwa miaka minne.
Hata
hivyo ombi lake lilikataliwa na maafisa wa uchaguzi, kwa misingi
kwamba anakabiliwa na mashitaka ya uhaini yanayohusiana na kipindi
chake cha utawala.
Hapo Jana mahakama mjini Islamabad iliamuru Musharraf akamatwe.
Post a Comment