Mbio za marathon zitakazofanyika
jijini London leo zimeandaliwa huku kukiwa na tahadhari kubwa ya usalama
kufuatia mashambulizi ya bomu yaliyozikumba mbio za marathon za Boston nchini
Marekani.
Milipuko hiyo miwili ambayo iliwauwa
watu watatu na kuwajeruhi wengi zaidi ya 180 mjini Boston Jumatatu wiki
iliyopita, imewalazimu waandalizi wa mbio za London kuimarisha mikakati ya
usalama katika jitihada za kuwapa matumaini wanariadha pamoja na takribani
watazamaji nusu milioni watakaojitokeza kushangilia mitaani.
Polisi zaidi watafanya doria katika
barabara itakayotumia kwa mbio hizo.
Serikali ya Uingereza imeahidi
kufanya kila iwezalo katika juhudi za kuhakikisha usalama wa wote
watakaoshiriki tamasha hilo maarufu.
Wanariadha watavaa vitambaa vyeusi,
wakati waandalizi wakisema kuwa euro mbili, na senti thelathini kwa kila
mwanariadha atakayemaliza mbio hizo zitatolewa kugharamia waathiriwa wa
mashambulizi ya Boston.
Post a Comment