Mvua kubwa inayoendelea kunyesha kote nchini Kenya yaendelea kusababisha maafa
huku vitengo vya serikali ambavyo vinavyoshughulikia matukio ya dharura
vikimulikwa. Hivi leo, watu wanane wameripotiwa kufa maji baada ya gari
walilokuwa wakisafiria kusombwa na mafuriko mjini Kargi kaunti ya
Marsabit. Haya yameripotiwa huku gari la abiria lilisombwa na mafuriko
wakati dereva alipojaribu kuvuka daraja lililokuwa limefurika na
kuharibika vibaya mtaa wa Nkoroi mjini Kiserian.
Post a Comment