Vodacom Tanzania na Fenix International zimezindua chaja mpya za simu 'Readysety' zinazotumia nishati ya jua na zenye uwezo wa kuchaji zaidi ya simu 5 tofauti kwa wakati mmoja


Mkuu wa Masoko wa Vodacom Tanzania Bw.Kelvin Twissa (kushoto)na mkazi wa Kibaha Bi Anna Joseph ambaye ni mmoja wa wadau walionufaika na huduma ya chaja za Readyset,wakiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) namna chaja hizo mpya na zinatumia nishati ya jua zinavyofanya kazi . Uzinduzi na hatimaye kuanza rasmi kwa matumizi ya kifaa hicho hususan kwa maeneo yaliyo nje ya gridi ya Taifa umefanyika Dar es Salaam kupitia ubia baina ya Vodacom Tanzania na Kampuni ya Fenix International. Wanaoshuhudia nyuma ni Meneja wa biashara wa kimataifa wa Fenix International, Peter Glenn, na Mkurugenzi Mtendaji wa Fenix International,nchini, Peter Mungoma.

Post a Comment

Previous Post Next Post