WANAFUNZI NA WALIMU 70 WAPATIWA MAFUNZO YA UKOCHA JIJINI ARUSHA

 
baadhi ya wanafunzi wakifanya mafunzo ya ukocha kwa vitendo yaliokuwa yakiendeshwa na kituo cha International Insparation kanda ya kaskazini kwenye viwanja vya sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
picha ya pamoja baada ya kumaliza mafunzo yao wakiwa na nyuso za furaha baada ya kutunukiwa vyeti na katibu wa baraza la michezo la taifa Henry Lihaya kwenye uwanja wa Seikh Amri kalita Abeid.
******
Na Mahmoud Ahmad Arusha
Mafunzo ya michezo shirikishi kwa jamii ya kukuza vipaji na michezo yaliokuwa yakindeshwa na kituo cha kuendeleza vipaji na michezo cha International Insparation kanda ya kaskazini kwa wiki moja na kuwashirikisha zaidi ya walimu na wanafunzi 70 yamefungwa jana jijini hapa na katibu wa BMT.
 
Akifunga mafunzo hayo katibu mkuu wa baraza la michezo la taifa Henry Lihaya aliwataka wanafunzi hao kujituma na kujijenga kwenye masuala ya kimichezo kwani kwa sasa michezo ni ajira tosha.

Huku akiwataka kuyatumia vizuri mafunzo hayo kwa manufaa ya taifa na kujenga miili yao sanjari na kupiga vita maambukizi ya magonjwa ya ukimwi na Malaria kupitia michezo watakayoenda kufundisha.

“Ndugu zangu vijana mkumbuke hivi sasa michezo ni ajira na mafunzo mtakayopata yatawajengea uwezo na msikae nayo muende mkafundishe kama mlivyofundishwa ilikupiga vita matumizi ya madawa ya kulevya na maradhi muwe mabalozi wazuri huko muendako”alisema Lihaya

Nae Mratibu wa Internation Inspiration mkoa wa arusha ambao wameratibu Mafunzo hayo Samwel Mpenzu alisema kuwa mafunzo hayo yaliwashirikisha zaidi ya walimu30 na wanafunzi 30 kutoka halmashauri ya jiji la Arusha na yalihusu kozi ya ukocha wa michezo mbali mbali ikiwa ni muendelezo wa kusogeza michezo kwa vijana.

Mpenzu alisema kuwa Ujumbe wa mafunzo hao ulikuwa ni michezo kwa Afya na kuwa mbali na mafunzo ya ukocha pia waliwafunza kujikinga na maambukizi ya maradhi wakiwa michezoni sanjari na ushirikishi wa jamii katika kukuza michezo hapa nchini.

“Unajua kuwa michezo ni huduma muhimu hivyo yatupasa kuwasogezea jamii kupenda michezo katika kupiga vita maradhi mbali mbali yanayoiandama jamii”alisema Mpenzu.

Aidha mwalimu wa mchezo wa riadha Francis John alisema kuwa katika mchezo huo alikuwa na wanafunzi zaidi ya 21 na walijifunza jinsi ya kutupa mitupo,Miruko,na Mbio na wote walifanikiwa kumaliza mafunzo hayo.

Mwanafunzi wa shule ya sekondari Felex Mrema Greygory John 15 alisema kuwa pamoja na kupata mafunzo hayo atayatumia vizuri kataka kuendeleza michezo hapa jiji na mkoani huku akiwataka vijana wenzake kuacha kutumia madawa ya kulevya kwani ni hatari kwa afya zao na huharibu maisha.

Post a Comment

Previous Post Next Post