![]() |
| Margaret Thatcher. |
Waziri Mkuu wa zamani kupitia chama cha Conservative, Margaret Thatcher amefariki dunia mapema leo baada ya kupatwa na kiharusi.
Waziri Mkuu huyo wa kwanza Uingereza na mwanamke pekee kiongozi wa
kisiasa amefariki akiwa na umri wa miaka 87, baada ya afya yake kuwa
ikizorota kwa zaidi ya muongo mmoja.
Msemaji wake Lord Bell alisema: "Ni kwa huzuni kubwa kwamba Mark
na Carol Thatcher wametangaza kuwa mama yao Baroness Thatcher amefariki
kutokana na kiharusi asubuhi ya leo".
Malkia amesikitishwa kusikia kifo cha Baroness Thatcher na Mtukufu
atatuma ujumbe binafsi wa rambirambi kwa familia ya marehemu, ilisema
taarifa ya Buckingham Palace leo.
Waziri Mkuu David Cameron alisema: "Ilikuwa huzuni kubwa
niliposikia kifo cha Thatcher. Tumepoteza kiongozi mkubwa, Waziri Mkuu
bora na Mwingereza halisi".
Alitarajiwa kurejea mapema kutoka ziara yake ya Ulaya mchana huu
kufuatia kifo cha Baroness Thatcher, ilisema taarifa ya Downing Street.
Binti wa kiongozi huyo, ambaye amekuwa Waziri Mkuu aliyekaa
madarakani kwa muda mrefu zaidi nchini Uingereza katika karne ya 20,
atazikwa kwa heshima zote za kitaifa kwenye kanisa kuu la Mt. Paul.
Tangu kifo cha Winston Churchill, hakuna mwanasiasa yeyote
aliyepatiwa heshima kama hiyo. Mazishi yake pia yalifanyika hapo mwaka
1965.
Habari zaidi zitakujia hapa hapa muda mfupi ujao.

Post a Comment