Na Juma Nyumayo, Songea
MKURUGENZI wa TAKUKURU, Dkt. Edward Hosea, amesema kanuni za utawala bora zikifuatwa na wananchi wote wakazitekeleza kutapunguza rushwa na kuleta maendeleo ya haraka.
Dkt. Hosea ameyasema hayo leo Manispaa ya Songea akitoa mada kwa viongozi wa Dini za kiislamu na kikristu wa zaidi ya 50 toka mikoa ya Iringa, Njombe na wenyeji Ruvuma katika Ukumbi wa Herritage Cottage, Manispaa ya Songea leo.
Amesema kuna mambo kadhaa yanayosababisha kuchochea rushwa ikiwa ni pamoja na mikataba ya kza kama ile ya kudumu na pensheni ambayo humfanya mwajiriwa kutoleta tija.
"hivi mtu ameajiriwa kwa Mktaba wa kudumu na pensheni ataleta tija huyu?, aliwauliza viongozi wa Dini na kuwatolea mfano wa wale wanaoajiriwa kwa mkataba wa muda mfupimfupi na kwamba mtu anaweza kuajiriwa tena kama ataleta tija na kuzingatia utawala bora kwa kuwahudumia wananchi.
Dkt. Hosea amekerwa sana na tabia ya wafanyakazi kutosimamiwa vizuri na viongozi wa kwa kuitwa "wanoko" na kuacha mambo yaende hovyo hovyo.
Angalia pale Dar es Salaam, watumishi wanakwenda kazini muda wowote na usitegemee tija pale," akaongeza kuwa hata viongozi wao wanaowasimamia hawawakalipii kwa kuogopa kuitwa wanoko.
Alisema hatamisikiti na makanisa kama hayatasimamiwa, na viongozi ambao wapo makini hayatasimama na hivyo nadiriki kusema Uongozi ni unoko wanaoukataa wafanyakazi wazembe.
akaendelea kusema ili kudhibiti rushwa kuna vigezo vya uwajibikaji, uwazi, ubashiri wa sharia, sera uwezo wa mtu binafsi, taasisi ni muhimu na kumalizia ushirikishwaji wa watu kuwa ni misingi muhimu.
Awali viongozi hao wa Dini walimbana maswali Dkt. Hosea kama kweli taasisis yake inawatumishi wasafi, jambo alilokiri kuwa baadhi siyo wasafi na kwamba tayari amekwisha wafukuza kazi watumishi 12 waliotuhumiwa kwa makosa mbalimbali.
amewathibitishia viongozi hao kuwa hivi sasa anajenga uwezo wa watumishi na taasisi yake kwa kuwapeleka watumishi katika masomo ya muda mrefu na mfupi pia kuwaboresha kimaslahi.
"jamani mkiwaona watumishi wetu wanavaa vizuri wanaendesha magari si kwa bahati mbaya na si wala rushwa tunawakopesha kuwapunguza tama," alithibitisha Dkt Hosea.

Post a Comment