Mwishoni mwa mwaka jana nilifanya interview na marehemu kuhusu maisha
yake,historia yake katika muziki na mipango yake katika muziki.Katika
interview hii marehemu alizungumza jinsi alivyoingia kwenye muziki,kundi
lake la chamber squad,album zake,tuzo na mipango yake kwenye muziki
ambapo ilikuwa ni kutoa
album ya 3.
album ya 3.
Ngwair alisema jina lake halisi ni Albert Kenethj Mangwair, asili yake
ni Ruvuma,alizaliwa Mbeya tarehe 16 November mwaka 1983 akiwa ni mtoto
wa mwisho kwa baba yake kama mtoto wa 10 na kwa mama yake alisema ni
mtoto wa 6.Albert Mangwea alizaliwa Mbeya baadae akahamia Morogoro
pamoja na familia, akasoma shule ya msingi Bungo hadi Darasa la 5 kisha
akahamia Dodoma pamoja na baba yake nakumaliza shule ya msingi Mlimwa
Dodoma.Alivyoenda Sekondari huko ndo alikutana na kina Mez B, Noorah na
masela wengine kisha kuanza muziki rasmi nakuweza kurekodi album ya
kwanza kama Chamber Squad iliyokuwa inaitwa 'Heshima kwa wote'.
Baadae alikuja Dar es salaam kisha baadae katika mishemishe za mjini
mchizi wake ambaye alikuwa ni msanii pia anayejulikana kwa jina la Tony
akaenda nae kwa Majani yaani Bongo Rec ambapo Majani akaona anauwezo
nakurekodi ngoma ya kwanza mwaka 2003 kama solo artist iliyokuwa inaitwa
'Geto langu' na ndo ukawa mtoko wa Ngwair.
Marehemua alisema mwaka 2004 ndo alitoa album ya kwanza 'AKA MIMI'
iliyokuwa na nyimbo kali kama 'SIkiliza', 'Mikasi' , 'Geto langu' na
nyingine kibao na album hii ilimpa tuzo ya Kilimanjaro kama album bora
ya Hip Hop,ilifanyika Bongo Rec.Album ya pili ilitoka mwaka 2009 iliitwa
NGE ilikuwa na nyimbo kama 'CNN', 'Nipe dili' wimbo ambao ulimpa tuzo
nyingine ya Kilimanjaro kama wimbo bora wa Hip Hop.
Katika interview hiyo Marehemu alimtaja msanii wa Tanzania aliyekuwa
akimsikiliza na alikuwa akimpenda kabla hajatoka na hata baada ya kutoka
ni Profesa Jay.Pia.Katika interview hiyo Ngwair alisema kuwa ana mtoto
mmoja.
*Marehemu Ngwair alisema kuwa hajawahi kuwa na bifu na msanii yeyote.
*Alipenda kujiita aka Cowboy kutokana nakupenda maisha ya Shamba.
* Marehemu alisema alisomea Ufundi katika chuo cha ufundi Mazengo,ufundi mwashi
*Alisema kuwa ana mtoto mmoja
SIKILIZA interview hiyo hapo chini From Anna Peter
Post a Comment