
MBUNGE wa Singida Mashariki, Tundu Lissu
(CHADEMA) amewataka wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mkwawa kutumia kura
zao vizuri katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 kwa kuiondoa madarakani
Serikali ya Chama Cha Mapinduzi kutokana na kudidimiza uchumi na
kutoleta maendeleo nchini.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara
baada ya kualikwa na Jumuiya ya Wanafunzi wa CHADEMA walioko mkoani
hapa, Lissu alisema Serikali ya CCM imeshindwa kumkomboa mwananchi
kutokana na wabunge na viongozi wake kutokuwa na uchungu na nchi.
Alisema ni kazi kubwa kwa sasa kwa
mwananchi kupata maendeleo chini ya CCM, hivyo ni jukumu la kila
mwananchi kuitumia kura yake kuwachagua wabunge wengi wa upinzani na
upande wa rais.
“Kila Mtanzania anajua kuwa utawala wa
CCM ni giza tupu, angalieni maisha ya walimu, askari, wakulima na
wafanyakazi, wako katika hali ngumu sana,” alisema.
Aidha, alitumia nafasi hiyo kumsifu
Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa kwa kazi anayofanya
katika kutetea maslahi ya taifa na Mkoa wa Iringa kwa ujumla kutokana na
kusimama kidete bungeni.
Post a Comment