Mabingwa wa soka wa Ujerumani Bayern Munich na Borussia Dortmund leo wanapambana katika fainali ya  kugombea kombe la klabu bingwa barani Ulaya itakayochezwa kwenye uwanja wa Wembley mjini London.
Bayern Munich iliitoa Barcelona ya Uhispania katika nusu fainali na Borussia iliishinda Real Madrid pia ya Uhispania.
Kocha wa Bayern Jupp Heynckes amesema fainali ya leo ni fursa yake ya mwisho ya kulitwaa taji la klabu bingwa za Ulaya-champions League.
Kwa upande wake kocha wa Borussia Jürgen Klopp amesema ni Bayern iliyojawa shinikizo ila wao hawana wasiwasi na ushindi katika mechi ya leo.