Majambazi yapora na kumuua mwanamke kwa risasi Dar

mwanamke-auawa-na-majambazi-pikipiki-kuporwa-aporwa-milioni-10-kumi
Majambazi yampora mwanamke ambaye jina lake halijapatikana kiasi cha shilingi milioni kumi na kumuua kwa kumpiga risasi. Majambazi hao walitokomea kusikujulikana muda mfupi baada ya kufanya tukio hilo,  lililotokea jana jioni saa 5:16 jioni.


Ushaidi ambao bado haujathibitishwa unasema mama huyo  alikua akitoka benki ya CRDB tawi la Uhuru. Majambazi hao waliokua wakimfuatilia kwa kutumia pikipiki. Dada huyo  alipotoka tu wakaligonga gari lake kwa makusudi na ndipo dada huyo aliposimama ili angaalie nani kagonga gari lake. Mmoja wa majambazi hao alishuka na kumpiga risasi ya kifuani na kutokomea na kiasi hicho cha pesa.
Mpaka sasa hatujapata habari yoyote kuhusu kukamatwa kwa wahalifu hao.
Chanzo: WilliamMaceleca

Post a Comment

Previous Post Next Post