Mama Asha Suleiman Iddi akabidhi madawati kwa skuli wilaya ya Kaskazini B

Meneja Biashara  kutoka makao makuu ya benki ya NMB Jijini Dar es Salaam Bibi Sheilla Senkoro akimkabidhi mgeni rasmi Mama Asha Suleiman Iddi madawati 100 na viti 100 kwa ajili ya skuli za msingi za Bumbwini na Mangapwani hapo skuli ya msingi Bumbwini Wilaya ya Kaskazini B

Taasisi za Umma,Mashirika pamoja na Sekta Binafsi zina wajibu wa kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali Kuu katika kuwajengea mazingira bora Wananachi wake hasa katika Sekta muhimu ya Elimu yenye dhamana ya kufinyanga   wataalamu na Viongozi wa baadae.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi alieleza hayo wakati wa hafla maalum ya kukabidhi meza na viti mia moja kwa skuli za msingi za Bumbwini na Mangapwani iliyofanyika katika skuli ya msingi Bumbwini iliyopo Wilaya ya Kaskazini “ B”.
Msaada huo wenye thamani ya shilingi za Kitanzania milioni kumi (10,000,000) umetolewa na benki ya NMB Tanzania, ambapo kila skuli imebahatika kupata meza hamsini na viti hamsini.
Mama Asha Suleiman Iddi alisema  nguvu za Endelea kusoma kwa kubofya hapa

Post a Comment

Previous Post Next Post