Risti ambazo wanadai kuwa wamekuwa wakitozwa faini kubwa ambazo kisheria haipo kabisa
Hali ya mgomo wa madereva
daladala katika Manispaa ya Iringa limechukua sura mpya baada ya
madereva hao kuamua kueleza uozo uliopo katika ofisi za Sumatra mkoa
wa Iringa kuwa amekuwa chanzo cha wao kunyanyasika.
Madereva hao wamesema kuwa
hawajapendezwa na utendaji kazi wa Sumatra ikiwa ni pamoja na kuondoka
mkoa wa Iringa kutokana na kushindwa kuifanya kazi hiyo kwa misingi
inayokusudiwa.
Madereva hao wametoa kilio chao
katika kikao cha kamati ya usalama barabarani kilichofanyika katika
ukumbi wa jumba la maendeleo mjini Iringa.
Kwani wamedai kuwa vikwazo mbali
mbali ambazo wamekuwa wakivipata madereva mjini Iringa vinasababishwa
na utendaji mbovu wa Sumatra mkoa wa Iringa pamoja na baadhi ya
askari wa usalama barabarani mkoa wa Iringa ambao wamekuwa
wakichangia kuwakandamiza zaidi.
Suala la kufutwa kwa stendi ya posta
na miyomboni kutakiwa kupita badala ya kuegesha daladala zao pia
limekuwa ni kikwazo zaidi kwa madereva hao na kuwa hawapo tayari
kuendelea kufanya kazi iwapo kiongozi huyo wa Sumatra mkoa wa
Iringa ataendelea kuwepo ofisini .
Awali mwenyekiti wa kamati ya usalama
barabarani mkoa wa Iringa Salim Abri Asas aliwataka madereva hao
kutuliza jazba na kueleza madai yao katika kamati hiyo ili kuyatafutia
ufumbuzi wa kudumu. |
Post a Comment