Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahaman Kinana akizungumza na
waandishi wa habari wakati wa mkutano wa wawekezaji wa sekta binafsi
(CEO Round Table Dinner) uliofanyika juzi usiku katika hoteli ya
Kilimanjaro Kempiski.
Na Mwandishi Wetu
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahaman Kinana amesema
ubinafsishaji haujafanikiwa vizuri kwani tangu sera hiyo ianze nchini
kuna viwanda havifanyi kazi wala kutoa ajira kama ilivyokusudiwa na
hivyo serikali ya Chama cha Mapinduzi inahitaji wawekezaji wa sekta
binafsi katika kuboresha huduma katika reli, barabara na viwanja vya
ndege.
Akizungumza
jana na waandishi wa habari, pamoja na wawekezaji wa sekta binafsi
katika mkutano ulifanyika juzi usiku katika hoteli ya Kilimanjaro
Kempiski.
Sera ya
CCM ipo wazi, tunawahitaji wawekezaji wa sekta binafsi na tumekuwa
tukiwahitaji tangu siku zote, lazima kwanza tutambue uwepo wao ili
tuweze kuwashirikisha katika sekta ya kusaidia jamii katika hhudma za
jamii
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi amezungumza na wawekezaji wa sekta binafsi,
mwezi mmoja tangu katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) naye kuzungumza na wawekezaji hao. Wakurugenzi hao hukutana na
vyama mbalimbali kujua sera zao vyama na ushirikiano wao na sekta
binafsi nchini.
Credits: Habarimseto blog
Post a Comment