SIMBA KUFUFUA AMA KUZIKA MATUMAINI YA NAFASI YA PILI? MGAMBO KUWASHUSHA POLISI NA TOTO RASMI?


Ligi kuu ya vodacom inataraji kuendelea kesho kwa kutegua vitandawili vya simba sc kufufua ama kuzika matumaini ya nafasi ya pili na ule wa Mgambo kuwashusha daraja rasmi Polisi Morogoro na Toto Afrika.
Kesho aliyekuwa bingwa wa ligi kuu ya vodacom Simba sc atawakaribisha Mgambo shooting ya Tanga katika uwanja wa Taifa, jijini Dar es saalam, ambapo ndio mchezo pekee utakao chezwa kesho.
Mchezo huo utakaoanza saa 10.30 viingilio vyake vita kuwa sh. 5,000 kwa viti rangi ya blue na kijani, sh. 8,000 viti rangi ya chungwa, sh. 15,000 kwa VIP C na B huku VIP A vikiwa ni sh. 20,000.
Katika mchezo huo Simba sc inahitaji kushinda ilikuimarisha mbio zake za kuifukuza Azam FC inayo kali nafasi pili. Simba ina pointi 42 na wanaiombea duwa mbaya Azam, ipoteze mechi zake mbili zilizo salia na wao washinde mechi zao mbili dhidi ya Mgambo hapo kesho na Yanga mei 18.
Simba inaweza kufikisha pointi 48, ambazo tayari Azam FC inazo. Ikiwa Azam itapoteza mechi zake mbili zilizosalia na Simba wakishinda michezo yake yote miwili, na kupelekea mshindi wa pili kuamuliwa kwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Wakati Simba wakihitaji ushindi wowote kufufua matumaini ya nafasi ya pili, wapinzani wao kwa mchezo wa kesho Mgambo shooting wanahitaji sare yoyote ile ili wajihakikishie kubaki ligi kuu ya vodacom huku wakiwashusha rasmi daraja Polisi Morogoro na Toto Afrika kuungana na African lyon.
Mgambo wanapointi 25 na wakitoka sare kesho watafikisha point 26 ambazo haziwezi kufikiwa na Polisi Morogoro na Toto Afrika wenye pointi 22 wakiwa katika nafasi ya 12 na 13.

Post a Comment

Previous Post Next Post