jinsi wanavyozifahamu timu za Simba na Yanga
wanaamua kuleta kikosi kizima ili waweze kushinda
mechi zao zote mbili.
Meneja wa Sofapaka, Ngalambe Roberto alisema watatua
nchini wakiwa na kikosi cha wachezaji 20 na
viongozi watato ambapo katika kikosi hicho watatua
na nyota wao wote.
"Sisi tumejiandaa vizuri tunazifahamu na kusoma
kwenye mitandao kuhusu timu hizi, hivyo tutakuja
na majeshi yote ili tushinde mechi zote mbili,"
alisema Ngalambe.
Alisema Tanzania kuna timu nyingi nzuri zenye
ushindani, lakini kwa Simba na Yanga ni zaidi,
hasa kutokana na upinzani mkubwa uliopo kwa timu
hizo mbili.
Waratibu wa mechi hiyo Kampuni ya Smartsports
wameziandalia timu za Yanga na Simba mechi ya
kirafiki dhidi ya Sofapaka kabla ya timu hizo
kwenda nchini Sudan kushiriki michuano ya Kombe la
Kagame.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Smartsports George
Wakuganda alisema baada ya Sofapaka kuwasili
jijini Dar es Salaam, itacheza mechi yake ya
kwanza Juni 12 dhidi ya Simba, itakayopigwa kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Alisema Juni 13, kikosi hicho kutoka Kenya
kitashuka tena uwanjani kuumana na mabingwa wa
Ligi Kuu Tanzania Bara na Afrika Mashariki (Kombe
la Kagame), Yanga.
Alisema mechi hiyo itakuwa nafasi nzuri kwa
mashabiki wa timu hiyo kuwaona wachezaji wao wapya
waliosajili kwa ajili ya msimu ujao, Mrisho Ngassa
na Amri Kiemba, kwa mara nyingine tena wakivaa
jezi za rangi ya njano na kijani.
Yanga hivi karibuni imewatangaza wachezaji wapya
wawili, wakitokea Simba, huku Haruna Niyonzima
akiongeza mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia
timu hiyo.
Post a Comment