Hali inaendelea kuwa si shwari kwa msanii Iryn Namubiru wa nchini Uganda ambaye anashikiliwa huko Japan kwa tuhuma za kupatikana na Dawa za kulevya baada ya uchunguzi kuonyesha kuwa unga wa ndizi aliokuwa amebeba ulikuwa umechanganywa na dawa hizo.
Katika tukio hili gumu, kitu kingine kibaya zaidi ni kwamba imefahamika kuwa, Promota Kim Ueno ambaye ndiye aliyeandaa onyesho la Iryn huko Japan kwa sasa anajiandaa kufungua kesi ya madai ya fidia kutokana na hasara aliyopata kwa msanii huyo kutokufika kwenye shoo.
Kutokana na sheria za Japan, mtu yoyote atakayepatikana na hati ya kosa kama
hili, ana uwezekano mkubwa wa kufungwa maisha na hata kuhukumiwa kifo,
kitu ambacho kinaongeza hofu ya hatma ya staa huyu wa Uganda.

Post a Comment