![]() |
| Wananchi wakishuhudia uharibifu baada ya shambulio la bomu. euronews |
Na Sabina Chrispine Nabigambo
Watu kumi na watano wamepoteza maisha na wengine zaidi ya thelathini
wamejeruhiwa nchini Libya katika Jiji la Benghazi baada ya kutekelezwa
shambulizi la bomu la kujitoa mhanga karibu kabisa na jengo la Hospital
ya Al Jala.
Naibu waziri wa mambo ya ndani Abdullah Massoud ndiye amethibitisha
idadi hiyo ya vifo huku akisisitiza kuwa hiyo ni idadi ya awali na
kwamba huenda idadi hiyo ikaongezeka ambapo tayari kidole cha lawama
kimeanza kuelekezwa kwa wapiganaji wanaomuunga mkono marehemu Kanali
Muammar Gaddafi.
Shambulizi hilo baya linakuja kipindi hiki ambacho kumekuwa na hali ya
taharuki ya usalama nchini Libya ambapo vituo vinne vya polisi tayari
vimeshambuliwa mjini Benghaz hivi karibuni viwili vikiwa vimeshambuliwa
Ijumaa iliyopita na vingine viwili vikishambuliwa siku ya Jumapili.
Baraza la usalama la umoja wa mataifa limelaani vikali shambulio hilo la
Benghaz huku wajumbe wa baraza hilo wakitilia mkazo wajibu wa jumuiya
ya kimataifa kuisaidia Libya kufanikisha mageuzi ya kupata demokrasia ya
amani na yakudumu.
Chanzo: kiswahili.rfi.fr

Post a Comment