STRAIKA wa Argentina Gonzalo Higuain huenda
akaangukia Arsenal na Kiungo wa Chelsea John Mikel Obi inasemekana ataenda Galatasaray ya Uturuki huku Man United ikidaiwa kuwapata Garay na Marchisio.
PATA ZAIDI:
Wenger na Higuain
Arsenal wako njiani kuvunja Rekodi yao ya Uhamisho na kumchukua Gonzalo Higuain toka Real Madrid kwa Dau la Pauni Milioni 25 ambalo litapita kiasi walicholipa kumnunua Mchezaji wao wa Bei ghali kabisa Andrey Arshavin waliemnunua kwa Pauni Milioni 15 Mwaka 2009.
Cha ajabu, Arshavin Mkataba wake unakwisha Juni 30 na Arsenal haipati hata Senti moja kwa vle anaondoka kama Mchezaji Huru.
Inasemekana Arsenal, baada ya kumpoteza Nahodha wao Robin van Persie aliekwenda Manchester United Msimu uliopita, sasa wako tayari kununua Majina makubwa ili wawe Washindani katika Ubingwa wa England ambao wameukosa tangu Mwaka 2004.
Higuaian yeye anataka kuihama Real ili apate Namba ya kudumu Timu nyingine ili aweze kuteuliwa Kikosi cha Argentina kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia Mwaka 2014 huko Brazil.
Mikel kwenda Galatasaray
Klabu ya Galatasaray wako njiani kumsaini Kiungo wa Chelsea Jon Obi-Mikel ambae ujio wa Meneja mpya Jose Mourinho umeonyesha yeye ni Mchezaji wa ziada.
Inatarajiwa Dili hii itakamilika baada ya Obi kurudi London akitoka huko Brazil ambako ameenda na Timu ya Taifa ya Nigeria kushiriki Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara yanayoanza leo Jumamosi Juni 15 na kumalizika Juni 30.
Obi alisainiwa Chelsea Mwaka 2006 na huyu huyu Mourinho akitokea Lyn Oslo ya Norway katika Uhamisho uliozua mgogoro mkubwa na Manchester United kwani Mchezaji huyo alikuwa tayari ameshasaini huko Old Trafford na Kesi hiyo kufika FIFA ambayo iliamua Chelsea lazima wawalipe Man United.
Garay
Kwa mujibu wa Mchezaji wa Benfica, Rodrigo, Mchezaji mwenzake wa Timu hiyo anaetoka Argentina, Ezequiel Garay, atanufaika sana akihamia Manchester United.
Garay, mwenye Miaka 26, alijiunga na Benfica Mwaka 2011 akitokea Real Madrid ambako hakuwa chaguo la Timu ya Kwanza lakini tangu atue Benfica amekuwa aking’ara.
Rodrigo ambae anatoka Spain amesema: “Kila Mtu anajua yeye ni Mchezaji hodari na mwenye akili. Kwa Miaka miwili akiwa Benfica ameonyesha hilo! Akienda Man United atakuwa bora zaidi!”
Marchisio
Huko Italy, upo uvumi mkubwa kuhusu Uhamisho wa Claudio Marchisio toka Juventus kwenda Manchester United huku Winga wa Timu hiyo Nani akiwemo kwenye Dili ya Uhamisho huo kwa kubadilishana ili aende Juventus.
Kiungo huyo kwa sasa yuko na Timu ya Taifa ya Italy kushiriki Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara yanayoanza leo Jumamosi Juni 15 na kumalizika Juni 30 huko nchini Brazil.
Inaaminika mwenyewe Claudio Marchisio anataka kuihama Juventus baada ya Klabu hiyo kushindwa kuboresha maslahi yake binafsi lakini Mabingwa hao wa Italy wanataka Dau la Euro Milioni 25 lakini Wachunguzi wanaamini Man United inaweza kuwapa Juve Fedha kidogo pamoja na Winga wao Nani.
Post a Comment