Baada ya Simba SC,Al Hilal,El Merreikh,Tusker FC,Nao Mabingwa watetezi wa kombe la Kagame Kutoenda Dafur kutetea Kombe Lake.

Yanga SC .

Siku chache baada ya Vilabu Vya Simba SC ya Dar es salaam,El MerreikhTusker F.C ya Kenya na Al Hilal kusema havipo tayari kushiriki michuano ya Kagame Cup iliyopangwa kupigwa nchini Sudan kwenye eneo la Darfur kwa kuhofia usalama wao,nayo Klabu wa Yanga SC  ambao mabingwa  watetezi wa kombe hilo la Kagame hawatoenda kushiriki michuano hiyo mwaka huu iliyopangwa kuanza hivi karibuni huko Darfur Sudan.

Habari za kuaminika kutoka kwa chanzo cha karibu na uongozi wa klabu wa Yanga kimesema Hatua hiyo inakuja siku chache baada ya serikali kupitia wizara ya mambo ya nje ya Tanzania kusema kwamba haioni busara kwa vilabu kwenda Darfur kwa sababu eneo hilo bado halina usalama wa kutosha - kauli iliyopelekea mwenyekiti wa klabu ya Simba Ismail Aden Rage kusema kwamba timu yake haitokwenda Darfur kushiriki michuano hiyo mwaka huu.

Tusker F.C.
Kwa mujibu wa CECAFA na chama cha soka cha Sudan ni kwamba michuano hiyo itachezwa kwenye lililo salama na lenye ulinzi mkubwa hivyo timu hazihitaji kuwa na wasiwasi juu ya usalama wao pindi watakapoenda kushiriki michuano hiyo mapema mwezi ujao.



Hatua ya Yanga SC kujitoa inazidi kuongeza idadi ya vilabu ambavyo vimesema ikiwa michuano hiyo itafanyika Darfur basi havitashiriki Kagame Cup mwaka huu, vilabu vikubwa vya Sudan AL Hila na El Merreikh, Tusker ya Kenya na Simba SC vyenyewe vilishatangaza uamuzi wa kutokwenda Darfur kwa ajili ya michuano hiyo. 

Juma Kaseja wa Simba SC.
Michuano ya Kagame safari hii imepangwa kufanyika katika miji ya Darfur ya Kaskazini pamoja na Gordofan ya Kusini Kuanzia Juni 18 mpaka Julai 2 mwaka huu ambapo kutakuwa na makundi matatu huku Kundi A likiwa na timu za Merreikh-Elfasher ya Sudan, APR ya Rwanda, Simba ya Tanzania na Elman ya Somalia. 


Wakati Kundi B litakuwa na timu za Al-Hilal-Kaduugle ya Sudan, Tusker ya Kenya, Al Nasir ya Sudan Kusini, Falcon ya Zanzibar na Al Ahly Shandi ya Sudan huku Kundi C likiwa na timu za Yanga ya Tanzania, Express ya Uganda, Ports ya Djibouti na Vital O ya Burundi.

Post a Comment

Previous Post Next Post