BALOZI KHAMIS KAGASHEKI AFUNGUA MKUTANO WA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA TANAPA MKOANI IRINGA



1aWaziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akifungua mkutano wa Shirika la Hifadhi za Mbuga za Taifa TANAPA na wahariri wa vyombo vya habari kuhusu Wajibu wa vyombo vya habari katika kukabiliana na Ujangili katika hifadhi za taifa unaofanyika kwenye ukumbi wa Siasa na Kilimo Ofisi za Manispaa ya Iringa.

 Balozi Kagasheki amewaasa wahariri wa vyombo vya habari kujadiliana kwa undani suala zima la kukomesha ujangili na jukumu la wanahabari katika mkakati huo wakishirikiana na serikali kwa ujumla kupitia taasisi za ulinzi katika mbuga za wanyama, amewataka wahariri kuwa wabunifu kwa kuandika makala na habari za kiuchunguzi ili kuibua mbinu hizo chafu na majangili ili kutokomeza ujangili huo na kupata ufumbuzi kamili wa changamoto hizo za ujangili.

 Ameongeza kwamba wizara yake iko tayari kupokea maoni mbalimbali kutoka kwa wahariri na wadau mbalimbali yatakayofanikisha kupata ufumbuzi wa kutokomeza kabisa ujangili katika mbuga na pia amejiwekea utaratibu wa kukutana na waandishi wa habari kila mwezi atakutana na vyombo vya habari ili kuzungumza na wanahabari kuhusu masuala mbalimbali ya wizara hiyo.
2aWahariri mbalimbali wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki wakati akifungua mkutano huo. 3aWahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa makini katika kusikiliza wakati Waziri Balozi Khamis Kagasheki akizungumza katika mkutano huo. 4aBalozi Khamis Kagasheki akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano huo kwenye ukumbi wa Siasa na Kilimo mjini Iringa 5aMkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma akizungumza katika mkutano huo wakati akimkaribisha Waziri wa Malisiali na Utalii Mh. Balozi Khamis Kagasheki.
1 Waziri wa Malisili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akiongozana na Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma wakati akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa Siasa na Kilimo mkoani Iringa ambako mkutano wa Wahariri wa vyombo vya habari na Shirika la Hifadhi za mbuga za Taifa TANAPA unafanyika. 3Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya bunge ya Ardhi Mazingira Ndugu James Lembeli akiingia kwenye ukumbi wa mkutano huku akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa TANAPA Ndugu Allan Kijazi kushoto. 4Waziri wa Maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki wa pili kutoka kulia akiwa katika mkutano huo kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi na Mazingira Ndugu James Lembeli na kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa TANAPA Ndugu Allan Kijazi na Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma. 5Waziri wa Maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki katikati akiwa katika mkutano huo kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya bunge ya Ardhi na Mazingira Ndugu James Lembeli na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma 6Waziri Kivuli wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa akizungumza katika mkutano huo huku Waziri wa Maliasili Balozi Khamis Kagasheki wa pili kutoka kushoto akisikiliza, wengine ni Ndugu James Lembeli Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi na Mazingira na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma. 7Mwenyekiti wa Kamati ya bunge ya Ardhi na Mazingira Ndugu James Lembeli akizungumza katika mkutano huo huku waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akisikiliza kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma. 8Mkurugenzi wa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akizungumza katika mkutano huo kukaribisha wageni mbalimbali waliohudhuria mkutano huo unafofanyika kwenye ukumbi wa Siasa na Kilimo mjini IringaPICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE- IRINGA

Post a Comment

Previous Post Next Post