Bolt tayari kwa mashindano ya Rome

Usain Bolt
Mwanariadha Usain Bolt, anayeshikilia rekodi ya dunia katika mbio za mita 100 na 200 anasema ana imani ataweka rekodi mpya ya mbio za mita 200 msimu huu.
Mjamaica huyo mwenye umri wa miaka 26 alishindwa na Mmarekani Justin Gatlin kwenye mbio za mita 100 mashindano ya Diamond League mjini Rome wiki iliyopita.
Sasa anajiandaa kwa mashindano ya Diamond Leage mjini Oslo hapo kesho, ambapo atashiriki katika mbio za mita mia mbili.

Mwanariadha huyo anakabiliwa na jeraha la mguu ambalo limemfanya kutoshiriki katika mashindano kadhaa mwaka huu, lakini ana matumaini ya kuwa katika hali nzuri kabla ya mashindano ya dunia yatakayoandaliwa mjini Moscow Urussii.
- bbc

Post a Comment

Previous Post Next Post