HATIMAYE
ndoto za kipa wa Kimataifa Mghana Yaw Berko kuendelea kuichezea klabu
ya Yanga zimefikia tamati baada ya kusajkiliwa kwa kipa mzawa,
Deogratius Munishi 'Dida'.
Hiyo
imetoa jibu la utata uliuokuwa umetanda ndani ya klabu hiyo baada ya
Berko kumaliza mkataba wake mwezi Mei na hivyo viongozi kuwa katika
mjadala juu ya kumuongeza ama kutomuongeza mkataba mpya.
Hata hivyo, habari ambazo Sports Lady Blog
imezipata kutoka Yangfa zinaeleza kuwa, kocha mkuu wa klabu hiyo Ernie
Brandts ndiye aliyekataa kuobngezwa mktaba kwa Berko na badala yake
kubariki usajili wa Dida.
Berko
ambaye alijiunga na Yanga mwaka juzi hakuweza kuichezea klabu hiyo
katika mzunguko wa pili wa ligi kuu bara msimu uliomalizika baada ya
kwenda nchini Congo kujaribu kujiunga na klabu ya FC Liupopo ya huko
ambayo ilipanga kumbadili na beki, Kabange Twite.
Hata
hivyo mazungumzo juu ya kubadilishana huko wachezaji hayakufikia
muafaka na ndipo Lupopo ilipomchukua Twite na Berko kurejea nchini
kuendelea kusubiri hatima yake.
Kusajili
kwa dida kunafanya Yanga kufikisha makipa watatu baada ya Ali Mustafa
;'Barthez' na Yusuf Abdallah ambaye amepandishwa toka kikosi cha Vijana
cha Yanga
Post a Comment