Chama
cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema kimeibuka jana bungeni na kusema
Serikali inafahamu ukweli wa mlipuko wa bomu uliotokea katika mkutano wa
chama hicho jijini Arusha.
Chama
hicho kimesema Serikali ilitumia kutokuwepo kwao bungeni kupotosha
wananchi kuhusu hali halisi juu ya mlipuko wa bomu hilo uliotokea wakati
chama hicho kikihitimisha kampeni zake za uchaguzi mdogo wa udiwani
katika Viwanja vya Soweto jijini Arusha, Juni 15, mwaka huu.
Akizungumza
kabla ya kuanza kuchangia muswada wa sheria ya fedha ya mwaka
2013/2014, Waziri kivuli wa Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi wa
Chadema, Halima Mdee alisema, “Kabla sijaanza kuchangia Mheshimiwa Spika
naomba nianze kwa kuwapa pole wakazi wote wa Arusha kutokana na mlipuko
wa bomu uliosababisha watu kupoteza maisha, kwani tangu limetokea tukio
hilo leo ndiyo nazungumza kwa mara ya kwanza,”
“Tunazilaani
kauli potofu zilizotolewa na Serikali hapa bungeni, Serikali inajua
nini kilichotokea Arusha na ilitumia kutokuwepo kwetu kupotosha,”
alisema.
Post a Comment