‘Big mechi’ ina siku yake
NINAYO furaha moyoni kukutana na wapendwa wa safu hii murua ili kuhabarishana mambo yahusuyo uhusiano na kuhakikisha neno mahaba lina kuwa na maana halisi. Nashukuru wote wanaoniunga mkono kuonyesha jinsi gani tupo pamoja.
Kama ilivyo ada nina imani mioyo yenu ina shauku kubwa ya kujua leo nimewaandalia nini? Natumaini kuwa chakula cha leo utakipenda, kazi yako ni kuandaa sahani na maji baridi ikiwezekana ongeza na ndizi au siyo wapendwa?
Mada yetu leo ni kuhusu kupanga siku ya mshike mshike, kama kukamua nazi basi tui liishe kwenye machicha hata ukikamua tena yatoke maji meupe. Sipendi kila siku kuliweka wazi kwa vile hii kona ya watu wazima wenye uwezo wa kutambua haraka kile tunachomaanisha.
Hii inatokana na tabia za rafiki yangu, kila siku kazini anasinzia asubuhi, ukimuuliza jibu lake kuwa ni mpambano wa jana ulikuwa mzito, shemeji yako ameniganda kama ruba. Mmh! Hii kali kila siku unataka kuikomoa, nani aliyekuambia alishawahi kukikomoa alichokikuta. Si wewe wa kwanza kukitumia, kilitumiwa na wahenga na wahenguzi hivyo kula saizi yako usitake kumaliza kilichojaa sahani.
Usiwe kama ndege aliyevamia shamba la mpunga akataka kumkomoa mwenye shamba matokeo yake alipasuka tumbo. Ndiyo maana nikaona kuna umuhimu wa kulielezea hili, si yeye tu, ni wengi wenye mtindo wa kumkomoa mwanamke au kukesha nayo. Kwa uchache naomba tuwe pamoja ili tupeane kidogo tulichonacho kwa manufaa ya wote.
Chakula cha roho au haki ya ndoa inatakiwa nafasi na uwezo wa wahusika wote. Hakuna mtu mwenye uwezo wa kufanya mapenzi ya nguvu kila siku, ila wapo wanaoweza kufanya mapenzi mepesi yasiyo na ushindani kila siku. Chozi moja la hamu kila siku inawezekana, wanawake wengine wameumbwa wakaumbika akilala, tena mlalo ‘unanitega’ bila kitu chochote mwilini, lazima upate kimoja.
Kwa makusudi anatangulia kulala ukifika kitandani ukiona tu roho haikupi, unatamani ulie angalau chozi moja ili ulale, mechi kama hizi huwa hazichoshi na huchezewa sehemu yoyote ile, jikoni, bafuni hata njiani. Ni za kawaida kama kusukutua maji na kutema.
Vile vile zipo mechi ambazo kila mmoja huweza kulia chozi moja au mmoja kumzidi mwenzie, mitanange ya aina hiyo ina uchovu wa kati, ambao huchezwa angalau mara mbili mpaka tatu kwa wiki.
Hizi huwa hazikuchoshi sana una uwezo wa siku ya pili kufanya shughuli zako bila tatizo, mipambano kama hii ndiyo huchezwa sana majumbani na haziwachoshi wapinzani.
Lakini zipo zile zinazoitwa ‘tafu game’ ambazo kuicheza lazima uwe fiti asilimia 80 mpaka 100, ukiwa chini ya 50 huwezi kucheza.
Najua una swali ni mechi gani hiyo inayotaka uwe fiti asilimia 100? Hii kama ya Simba na Yanga, Manchester na Chelsea au Real Madrid na Barcelona, hapa ni kukamiana kila mmoja anataka kumuonyesha mwenzie yeye ni nani ana uwezo wa aina gani kumkata kiu ya mapenzi mpenzi wake.
‘Big mechi’ kama hii ina matokeo kidogo makubwa kila mmoja huweza kulia zaidi ya mara tatu na kuendelea inategemea na uwezo wenu. Mchezo huu unataka nafasi ili kila mmoja aonyeshe uwezo wake wa kulizungusha duara kubwa.
Michezo ‘tafu’ kama hii huwa haichezwi katikati ya wiki mara nyingi huchezwa siku ambayo wote siku ya pili mpo nyumbani hata mkikesha siku ya pili hamuendi popote mnaweza kushinda mmelala. Mchezo huu unahitaji maandalizi ya kiakili na kimwili kwani kila mmoja lazima ajue usiku hakuna kulala na mtoto hatumwi dukani.
---------- xxxxxxxxxxxxx ------------
ASUBUHI siku ya mpambano lazima mpeane tahadhari kwa maneno yenye kuchochea kila mmoja awe na hamu ya kushinda, utapomwambia mwenzio: “Leo nakusubiri usijichoshe ukasingizia kwa uchovu,” nina imani atakuwa na hamu ya mechi.
Jioni ya siku husika muoge pamoja ili kuongeza msisimko, ikiwezekana hata akiomba alie chozi moja bafuni mnyime ukimwambia subiri mpambano.
Mkitoka kuoga nina imani muda huo chakula kipo tayari hatuangalii kimeandaliwa juu ya meza kwenye mkeka au gunia, kona hii inamgusa mtu wa aina yeyote mwenye kipato cha juu na chini. Siku zote penzi halilindwi na wadhifa, cheo, fedha au uzuri wa sura, penzi ni wewe mwenyewe utakavyojitoa.
Mkishapata chakula ambacho siku hiyo mtalishana kama ndege na mwanaye, vitu hivi huongeza moto wa mpambano. Vile vile uongeza mapenzi ndani ya mioyo yenu na kuwafanya muondoe uoga wa homa ya mpambano.
Chakula chenyewe cha siku hiyo kiwe chepesi kinachoweza kukupa uwezo wa kufanya vitu vyako bila tatizo lolote. Pia hutakiwi kushiba sana ili kuupa mwili wako uwezo wa kujitawala kwa mapana zaidi.
Mkishamaliza kupata chakula mnatakiwa kupumzika kidogo ili kukifanya chakula kishuke sehemu zake. Wakiti mkiwa kwenye hati hiyo si vibaya mkaliwazana kwa mmoja kumlalia mwenzie huku mkiipa uhuru mikono yenu ivinjari miili yenu bila pingamizi lolote.
Nina imani sina haja ya kuzielezea sehemu zinazo takiwa kuguswa ili kuufanya mwili usisimke kujitayarisha kwa ajili ya mechi. Ukijua kuzigusa sehemu muhimu utasikia tu hata mihemo inabadilika. Kila mmoja ana sehemu zake ambazo lazima uzijue ili usiusumbue mwili wa mwenzio kugusa sehemu zingine zitakazompa karaha.
Baada ya kuhakikisha kuwa miili yenu imechemka asilimia 100, kwani kila mmoja atakuwa anahema katika hali isiyo ya kawaida, hata sauti zitakuwa zikitokea puani na mihemo ndiyo inatawala.
Hapo kila mmoja huwa na hamu na mwenzie, hicho ndiyo kipindi kizuri cha kuanza mpambano, hii husaidia kutochelewa kufika kileleni huku mkifurahia raha ya mapenzi yasiyoisha hamu.
Zoezi hili la kuuandaa mwili kabla ya mpambano si kwa tafu gemu pekee bali hata kwa mechi yoyote ile, kwani kuandaa mwili kuna faida kubwa, ipo siku nitaliongelea hili kwa undani zaidi.
Hapa sasa ndiyo sehemu ya kumaliza ufundi wako wote, lakini lengo likiwa ni kumkata kiu mpenzi wako. Mwenye nafasi ya kuutawala mchezo sehemu kubwa ni mwanaume, lazima uwe mtundu wa kuhakikisha unampa mitindo yote uijuayo, nina imani katika 10 ipo miwili mitatu itakayomgusa na kukuomba uirudie tena.
Kwa vile mmepania kukatana kiu hampumziki mpaka wote mhakikishe mmefika mwisho wa safari. Kuna baadhi, akishafika yeye hamkumbuki mwenzie akimwacha kwenye hali mbaya, wenye tabia hii hasa ni wanaume.
Mwanamke kama hujafika, usikae kimya ukiugulia moyoni, mshike mwambie “Usishuke mwenzio bado ndo kwanza zinakuja.” Nawe msindikize mwenza mpaka afike mwisho wa safari.
Baada ya safari ndefu yenye vilio na raha zisizo kikomo, mtapata mapumziko kisha mtaendelea. Hapo hakuna kulala mpaka majogoo. Lakini wapo wanaokwenda mwendo mfupi na wengine mrefu.
Mechi kama hizi si vibaya mara moja au mbili kwa mwezi na si kila siku mkirudi mnataka kukomoana, chakula kitamu huliwa kwa hamu kwa kuwa tamu ikizidi hukinaisha. Siyo kila siku ukienda kazini, unashindwa kuwa makini kwenye ajira yako ukitawaliwa na uchovu na usingizi, hali ambayo inaweza kumkumba mwezio.
Namalizia kwa kusema Big Mechi zinataka maandalizi ya kina ili kuhakikisha kila mmoja anafikisha alichokikusudia kwa mwenzake, hakikisha umemkata kiu mpenzi wako na kila mmoja atoe asante zisizo na idadi.
“Asante mpenzi leo umezikamua zote hapa najiona mwepeeeeesi.”
Mmh! Kwa sasa inatosha tukutane tena baadaye
By: Adinani K. Kwangaya
0657 666800
Post a Comment