HIVI NDIVYO SIFA UNITED ILIVYOIADHIBU MTAKUJA 5 - 2 AIRTEL RISING STARS


 Mshambuliaji wa Sifa United Haruna Athuman (kushoto) akichuana na Alex Simenga wa Mtakuja Beach wakati wa mechi ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars, mkoa wa Kinondoni, iliyochezwa kwenye uwanja wa Mwanamanyala Shule ya Msingi jijini Dar es Salaam leo Juni 24, 2013. Sifa United walishinda 5-2.
 Alphonce Shabani wa Mtakuja Beach (kulia) akimtoka Haruna Athuman waf Sifa United wakati wa mechi ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars, mkoa wa Kinondoni, iliyochezwa kwenye uwanja wa Mwanamanyala Shule ya Msingi jijini Dar es Salaam leo Juni 24, 2013. Sifa United walishinda 5-2.
Abdulazizi Haruna wa Mtakuja Beach na Hamir Sheh wa Sifa United wakiwania mpira wa juu wakati wa mechi ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars, mkoa wa Kinondoni, iliyochezwa kwenye uwanja wa Mwanamanyala Shule ya Msingi jijini Dar es Salaam leo Juni 24, 2013. Sifa United walishinda 5-2.

Baada ya kubamizwa 3-1 na Makumbusho United siku ya Jumapili Sifa United ya Manzese jana ilisahihisha makosa yake na kuiadihbu Mtakuja Beach 5-2 katika michuano ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka U-17 ya Airtel Rising Stars, mkoa wa Kinondoni, kwenye uwanja wa shule ya msingi Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Sifa United walianza mashambulizi mara tu baada ya kipyenga cha kwanza na kufanikiwa kupata goli la kwanza dakika ya tatu kupitia kwa Karim Athuman aliyeachia shuti kali na kumshinda golikipa wa Mtakuja Beach. Kabla vumbi halijatulia, Sifa United walifanya shambulio jingine la nguvu na kufanikiwa kuandika goli la pili mnamo dakika ya sita kupitia kwa Mustafa Yusuf.

Timu hiyo ya Manzese uliutawala mchezo katika kila idara na kufanikiwa kupata goli la tatu dakika ya 25 kupitia kwa Jumbe Evon ambaye aliwatoka walinzi wa Mtakuja Beach na kuukwamisha mpira wavuni huku akishangiliwa na washabiki wa timu hiyo. Baada ya hapo, Mtakuja Beach walikuja juu na kufanikiwa kupata goli dakika ya 39 kupitia kwa Alex Simega. Hadi mapumuzika magoli yakuwa  3-1.  

Baada ya kutoka mapumuziko, Sifa United waliendelea kulisakama lango la Mtakuja Beach na juhudi zao zilizaa matunda tena katika dakika ya 53 ambapo mshambuliaji Mustafa Yusuf alifunga goli la nne kabla ya Mtakuja kufunga goli la pili dakika ya 75 kupitiia kwa Steven Munyu.

Mchezaji wa Sifa United Mustafa Yusuf ambaye alikuwa nyota wa mchezo huo alidhihirisha umwamba wake pale alipofunga goli lake la tatu yaani ‘hat trick’ katika dakika ya 81 baada kugongeana vema na washambuliaji wenzake. Kufuatia ushindi huo Sifa United kesho Jumanne itapambana tena na Makumbusho na mshindi wa mchezo huo ndio atakayetawazwa kuwa bingwa wa ARS mkoa wa Kinondoni 2013.

Programu hii ya Airtel Rising Stars ni ya Afrika nzima likiwa na lengo la kuendeleza na kukuza  mpira wa miguu katika bara la Afrika kwa vijana wanaochipukia waweze kupata nafasi ya kuendeleza vipaji vyao.

Fainali za ARS Taifa vile vile zitatumika kuchagua timu bora za wavulana na wasichana ambao wataiwakilishaTanzania katika mashindano ya kimataifa ambapo nchi mwenyeji wa michuano hiyo itatangazwa mwezi ujao. Wachazeaji wengine watachaguliwa kwenda kwenye kliniki itakayoendeshwa na makocha kutoka klabu maarufu duniani ya Manchester United

Post a Comment

Previous Post Next Post