Jokate aongea baada ya Diamond kukiri kuwa anajuta kumkosea na kuuvunja moyo wake

Hivi karibuni Diamond aliamua kuweka ‘ego’ pembeni na kukiri kuwa Jokate Mwegelo ndiye msichana katika maisha yake aliyemkosea sana na anajuta kumuumiza
Diamond alifunguka hayo kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV, kilichorushwa wiki iliyopita.

Akiongelea jinsi alivyomuumiza Jokate, Diamond alisema, “Kwasababu alikuwa too innocent halafu hakuwahi kunikosea kitu chochote Jokate kabisa, halafu nikamwingiza kwenye matatizo, watu wakamchukulia tofauti kwamba ‘Jokate kamchukulia Wema boyfriend wake’ wakati nilimfuata mimi kama mimi, nilimtafuta mwenyewe halafu then nikawa niko naye halafu ghafla nikarudisha mahusiano kwa Wema. Sikujiskia vizuri halafu still haikuwa vizuri so sometimes nikikaaga hivi nasema nilimkosea.”

Akijibu swali la kwanini alimuacha Jokate, Diamond aliongeza, “Sijui nilirogwa hata sijui, I don’t know, sijui hata kwanini, hakuwahi kunikosea chochote sio, sababu nilikuwa nikikaa naye alikuwa akinishauri vitu vingi vya maendeleo, sijui ulikuwa ni utoto sielewi yaani, sijui ni kitu gani, nilijikisa vibaya sana, halafu mtoto wa watu mstaarabu sana, alijitahidi kujenga career yake sasa hivi imekaa vizuri.”

Bongo5 imewasiliana na Jokate ili kutaka kufahamu upande wake baada ya kusikia kauli ya Diamond aliyesema anafurahi kuona Diamond amefunguka ukweli.

“Watu wengi hawajui the real issue, I’m glad kama ame-acknowledge I was innocent in that whole matter,” amesema Jokate.

Post a Comment

Previous Post Next Post