Kampuni ya Bia ya Serengeti Yatunukiwa Cheti cha Viwango Kimataifa

Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Taylor pamoja na Meneja viwango wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Paul Kitambi wakionesha cheti walichotunukiwa na Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO) kwa wana habari jana katika ofisi za kiwanda cha bia cha Serengeti jana jijini Dar es Salaam.

Meneja viwango wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Paul Kitambi, akizungumza na wana habari, kuhusu kutunukiwa cheti 9001:2008 na shirika la viwango la kimataifa (ISO) baada ya kukidhi vigezo vya shirika la Det Norske Veritas (DNV) linaloaminika kimataifa katika kutoa huduma za ukaguzi na uhakiki wa utendaji wa viongozi na wafanyakazi katika makampuni, mkutano huo ulifanyika jana katika ofisi za Kiwanda cha bia cha Serengeti jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Taylor.
Meneja viwango wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Paul Kitambi akiwa amebeba cheti walichotunukiwa na Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO) mara baada ya kumaliza mkutano na wanahabari jana jijini Dar es Salaam.
Cheti walichotunukiwa na Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO) kinavyoonekana pichani.
Short URL: http://www.thehabari.com/?p=33870

Post a Comment

Previous Post Next Post