[ Mwandishi: Mwanne Othman]
Karamu ya bi Kidude kufanyika wiki ijayo
Mjukuu wake athibisha
Na Mwanne Othman
Karamu [Arobaini] ya msanii Nguli
katika tasnia ya wa muziki wa Taarab asilia na Unyago Fatma Bint Baraka
maarufu Bi Kidude aliyefariki dunia April 17 mwaka huu inatarajiwa
kufanyika wiki ijayo imefahamika.
Kwa mujibu wa mjukuu wa marehemu Bi Kidude Omar Kana tayari walishamfanyia kisomo kidogo ambacho kilifanyika May 26 mara tu baada ya kutimiza siku kamili 40 toka kufa kwake, hivyo kwakuwa Bi Kidude alikuwa na msanii mkubwa hapa nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla watafanya tena Karamu kubwa itakayofanyika wiki ijayo.
“Bado tupo kwenye maandalizi ya mwisho kwa ajili ya karamu ya Bi Kidude hivyo mara baada ya kumaliza vikao nitakufahamisha ni lini na saa ngapi Karamu hiyo itafanyika” alisema Omar mjukuu wa Bi Kidude.
Bi kidude alifariki dunia kutokana na maradhi ya Kisukari na Uvimbe Tumboni vilivyokuwa vikimsumbua kwa muda mrefu na alizikwa katika kijiji cha Kitumba wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja.

Post a Comment