Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Nape Nnauye.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeitakia kila la kheri timu ya Taifa Stars ambayo inacheza  kutafuta tiketi ya kucheza kombe la dunia mwaka 2014.
Taifa Stars katika mechi yake ya leo itavaana na Timu ya taifa ya Morocco.
Akizungumza kutoka Dar es salaam, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Nape Nnauye amesema CCM inaitakia kila lakheri Taifa Stars na mafanikio katika mchezo wa leo na kwamba CCM inatambua umuhimu wa taifa Stars kushinda mechi hiyo.
Ameongeza kuwa anaamini dua za CCM na Watanzania wote zitaiwezesha Taifa Stars  kushinda mechi yake dhidi ya Morocco.
“Watanzania tunaomba muiombee Taifa Stars, tunaimani nayo, bila shaka itashinda leo” amesisitiza Nape