MANUEL PELLEGRINI KOCHA MPYA WA MAN CITY

 - MSOMI ALIYE TAYARI KUPANDIKIZA FALSAFA ZAKE ZA KISOMI NDANI YA MANCHESTER CITY



Miaka 12 iliyopita, klabu ya Argentina San Lorenzo ilikuwa ikihitaji ushindi katika mchezo wa mwisho wa ligi ili kushinda ubingwa wa nchi hiyo. Manuel Pellegrini, kocha wa timu hiyo aliutumia usiku wa siku ya kuamkia mechi akisoma kitabu kwenye chumba kimojawapo kwenye kambi ya klabu hiyo. Umakini wake kwenye kusoma kitabu ulikatishwa, Fabricio Coloccini, wakati huo akiwa na miaka 19 akiichezea timu hiyo kwa mkopo, alikuwa akitoka chumbanikwake na kutembea kwenye korido, akionekana mwenye mawazo na hivyo kushindwa kulala, pia alikuwa na wasiwasi hata akashindwa kukaa chini akabaki anatembea tembea tu. 
Coloccini akiwa na wachezaji wa San Lorenzo wakishangilia

Pellegrini akuweza kuinuka kutoka alipokaa kwenda kumtuliza mlinzi huyo wa kiargentina bali alimwambia: "Fabricio, acha kuwa na wasiwasi kuhusu kitu chochote. Tumeshajitahidi na kufanya vizuri msimu wote, hivyo haitokuwa jambo kubwa sana kama tukichukua kombe au tusichukue."

"Unamaanisha nini?" Coloccini aliuliza. "Namaanisha kwamba - timu yetu ni bora kuliko zote, hilo ndio jambo muhimu, hivyo sijali kama tutashinda au kufungwa kesho."

Coloccini hakuweza kuamini maneno aliyokuwa akiyasikia kutoka kwa kocha wake. Alishangazwa sana na kauli za mwalimu wake kiasi akashindwa hata kujibu, alirudi chumbani kwake na kulala. Siku iliyofuatia wakaenda uwanjani na wakashinda mechi kisha kubeba ubingwa - na hapo ndipo Coloccini alipoona namna maneno ya Pellegrini yalivyomtuliza na kumfanya kucheza bila wasiwasi na matokeo kuisadia timu yake kubeba ubingwa. Kuna makinda wengi katika kikosi cha manchester City ambao watakuwa chini ya Pellegrini baada yaMuargentina huyo kutua Etihad - ambao watafaidi matunda ya falsafa ya saikolojia za kocha huyu.

Mapema mwezi huu, Pellegrini aliwahutubia makocha takribani  900 katika mkutano wa kimataifa wa makocha uliofanyika Malaga - Spain. Aliongolea mbinu anazotumia zilizomfanya aweze kuifikisha Malaga katika robo fainali ya Champions League msimu uliopita -- kwa bahati mbaya dakika mbili za nyongeza ziliinyima timu yake nafasi ya kwenda kucheza nusu fainali baada ya kufungwa walioinga fainali. 

KUHUSU FALSAFA ZAKE

"Kuna vitu vitatu muhimu ninavyohitaji kutoka wachezaji wangu; heshima, kujitolea/kujituma na kiwango kizuri," aliiambia Diario Sur. "Nina imani kwamba nitaweza kuingiza staili yangu ya soka katika nchi ya tano ambayo nitakuwa nafundisha soka ndani yake."

Pellegrini alianza maisha yake ya soka kwa kuichezea klabu ya Universidad de Chile, ambapo ilionekana wazi kwamba ujuzi wake wa kuwasoma na kuwaelewa watu utampeleka mbali. Alikuwa ndio mchezaji pekee aliyekuwa akisoma chuo kikuu -- alikuwa akichua engineering at Universidad Catolica -- na alikuwa mmoja kati ya wachezaji maarufu sana katika kikosi cha timu yao.

"Alikuwa mwanafunzi wa daraja la juu," anakumbuka mchezaji mwenzie Jorge Luis Ghiso, "lakini kila mtu alimheshimu na kumpenda." aliweza kuwafanya wakufunzi wake wamruhusu kuondoka darasani dakika 15 kabla ya muda ili asiwe anachelewa vipindi vya mazoezi.

Pellegrini ni mtu anayeenda na muda sana. Wakati alipotajwa kuwa kocha wa klabu ya Ecuador Liga Deportiva Universitaria de Quito, wachezaji wengi wenye makubwa walichelewa kufika mapema kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya timu moja ya mtaani - Pellegrini akawafungia mlango katika chumba cha kubadilishia nguo na kisha kukataa kuwaruhusu kucheza. Hawakuwahi kuchelewa tena sio mazoezini wala kwenye mechi. Ikiwa kocha aliyepita wa City Roberto Mancini aliiongoza timu hiyo kwa ubabe kwa wachezaji wake, Pellegrini anapendelea kuongoza kwa heshima kutoka anaowaongoza. 

"Inabidi uonyeshe kwamba una mamlaka ya kuwa kocha, lakini naweza kuwa dikteta na pia mwana demokrasia" alisema. "Dikteta kwa sababu wachezaji wanapaswa kukuheshimu, lakini kidemokrasia kwa sababu inabidi niwashawishi kama nahitaji wao wafanye hivyo."

City walisema sababu nyuma ya kufukuzwa kwa Mancini zilikuwa ni kushindwa kupata mafanikio waliojipangia (ukiachana na kufuzu kwa Champions League) na pia katika kauli hiyo hiyo walisema wanahitaji kuboresha kwa ujumla maendeleo ya klabu.

CEO wa zamani wa City Garry Cook aliiambia BBC kwamba maboresho yaliyohitajika hasa kutoka kwa mwalimu ni  - uelewa mkubwa za meneja kuifanya timu kuwa mali ya umma...kujieleza mbele ya vyombo vya habari...kuendesha biashara kwa kuwa na management nzuri katika masuala ya fedha katika kila wanachokifanya. Kwa ujumla ni kuelewa namna soka la kisasa linavyotaka kuendeshwa kibiashara, na sio timu kushinda tu mechi."

Uteuzi wa Pellegrini ni uamuzi mwingine muhimu uliofanywa na viongozi wapya wa kihispaniola - kama walivyoamua kuwekeza kwenye soka la Marekani kwa kuunda  New York City FC, klabu mpya MLS iliyoundwa kwa kushirikiana na New York Yankees, ni uamuzi unaoweza kuipeleka City hatua nyingine katika mahitaji yao ya kuteka soka la ulaya na kupata umaarufu mkubwa duniani kote.

Pellegrini, ambaye ni msomi mzuri sana hata kwenye mambo ya biashara na masoko ndio mtu sahihi wa kuitoa City ilipo kwenda hatua nyingine. Tabia yake ya kujisomea vitabu mbalimbali huwa inamsaidia katika maarifa ya ndani na nje ya uwanja. Kitabu ambacho alikuwa anasoma wakati Coloccini anahangaika na kushindwa kulala kule Argentina - kilikuwa kinahusu ni namna gani mtu au taasisi inaweza kuendelea kwenye masoko.

Post a Comment

Previous Post Next Post