Wizara ya sheria nchini Marekani imeanzisha uchunguzi kwa kile inachosema ni ufichuzi wa taarifa za siri uliofanywa na mtaalamu wa zamani wa mitambo wa Komputa katika shirika la ujasusi wa Marekani Edward Snowden.
Bwana Snowden alijitambulisha baada ya kufichua kuwa mashirika ya ujasusi nchini Marekani hufanya udukuzi kote duniani kwa kutumia mbinu ya kiteknolojia ya siri kuchunguza mawasiliano ya simu ya watu, barua pepe na mawasiliano mengine.
Ufichuzi wa Edward Snowden kuhusu shughuli hizo za kisiri zinazojumuisha kudukua mitandao yainternet na mawasiliano ya simu, umezusha wasiwasi kote ulimwenguni kuhusu kiwango cha ukusanyaji wa taarifa hizo za kijasusi Marekani.
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, William Hague, anatarajiwa kutoa tamko rasmi bungeni baadaye leo kuhusu tuhuma kwamba mashirika ya kijasusi Uingereza yalitumia data iliyokusanywa namashirika ya kijasusi Marekani kubadili sheria kali nchini humo kuhusu taarifa za siri.
Kwenye mahojiano na jarida la Guardian,Edward Snowden , alisema kuwa wamarekani, wanahujumu mamlaka ya serikali na kutishia demokrasia.
Hatua ya Snowdon, imesababisha wasiwasi kuhusu uwezo wa Marekani kukusanya taarifa za kijasusi ambao anasena ni mkubwa mno.
Aliambia jarida hilo kuwa jambo inalofanya Marekani ni la kutisha akiongeza kuwa wao huvamia mitandao na pindi mtu anapowasha mtambo wake wanaweza hata kuutambua mtambo wenyewe na mtu anayeutumia. Alisema kuwa mtu hawezi kuwa salama licha ya ulinzi unaotoa ili kuzuia uvamizi wa mitandao.
Aidha alisema kuwa ''sitaki kuishi katika jamii ambayo inafanya mambo kama haya., sitaki kuishi katika jamii ambayo kila ninachokisema kinarekodiwa.''
CREDIT TO BBC SWAHILI
Post a Comment