MISS KANDA YA NYANDA ZA JUU 2013 KUPATIKANA JUMAMOSI HII

  Kinyang’anyiro cha kumpata Miss Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kinatarajiwa kufanyika kesho katika ukumbi wa Mikutano wa Mtenda SunSet uliopo Soweto Jijini Mbeya.   Mratibu wa Shindano hilo Fredy Herbet, amesema baada ya warimbwende kutoka Mikoa yote inayounda Kanda kukaa kambini tangu Juni 25, Mwaka huu na kupata mafunzo mbali mbali wanatarajia kuivunja Juni 29, Mwaka huu baada ya Msindi kupatikana.   Ameongeza kuwa Shindano hilo limeandaliwa na Lake Victoria Arts & Culture Promotion chini ya Udhamini wa TBL kupitia kinywaji chake cha REDDS, SBC kupitia  Mountain Dew, Man Company, My Choice Botique, Ebony Fm na Bomba Fm radio.   Amesema kinyang’anyiro hicho kitasindikizwa na burudani kutoka kwa bendi ya FM Academia ya Jijini Dar Es Salaam na kuongeza kuwa kiingilio kitakuwa  shilingi 10,000/= kwa watu wa kawaida na 25,000/= kwa VIP.   Amewataja washiriki wanaong’ang’ania kuibuka kidedea kwa kuiwakilisha Kanda katika shindano la kumpata Miss Tanzania Mikoa wanakotoka kwenye mabano na namba aliyoshinda Mkoani kwake  kuwa ni pamoja na Lina J. Allan (Rukwa 1), Aneth B Mapugilo(Mbeya 2), Jesca Mikambi(Katavi 2), Nuru Baraka ( Katavi 1) na Neema Mality (Iringa 1).   Wengine ni Lucy George (Iringa 3), Nuriath Suleiman (Njombe 1), Evamary Gamba( Rukwa 2) Lilian Samson (Iringa 2), Naba Magambo (Mbeya 4), Jacklin J Luvanda (Mbeya 1) na Winfrida Felix Miss Njombe namba 2.   Kwa Upande wake Mwalimu wa Walimbwende hao Naomi Jones  ambaye ndiye anayeshikilia taji hilo amesema kambi iko vizuri na washiriki wote wanafuata maelekezo vizuri hivyo Majaji wawe makini kumtafuta Msindi kutokana na wote kuwa na sifa zinazofanana.
Na:Mbeya yetu

Post a Comment

Previous Post Next Post