MSIBA; ABDALLAH MSAMBA ALIYENG'ARA SIMBA SC, PAN NA SIGARA AFARIKI DUNIA USIKU WA KUAMKIA LEO MBEZI


Abdallah Msamba (katikati) akiwa na Emma Peter kushoto na Julius Mwakatika kulia enzi za uhai wake katika kikosi cha Sigara FC
Na Mahmoud Zubeiry,
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba SC ya Dar es Salaam, Abdallah Msamba amefariki dunia usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake Mbezi, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa mchezaji mwenzake wa zamani wa Simba SC, Madaraka Suleiman ‘Mzee wa Kimyinio’, Msamba alifariki usiku manane na taarifa wamezipata kutoka kwa mke wake.
“Babu Msamba hatupo naye, nimetoka kupigiwa simu na Kipese (Thomas) sasa hivi, kwamba kapigiwa simu na mkewe juu ya msiba wa Msamba,”alisema Madaraka ambaye alicheza naye Msamba Kajumulo WS na Simba SC.
Madaraka alisema kwamba kwa sasa wanakusanyana rafiki zake ili kukutana na mke wa marehemu kupanga taratibu za mazishi ya Msamba.
Msamba ni mmoja kati ya washambuliaji bora wa pembeni kuwahi kutokea Tanzania ambaye alikuwa ana nguvu, kasi na uwezo mkubwa wa kufunga mabao.
Kisoka aliibukia Pan African pamoja na akina Bakari Malima, Thomas Mashalla, Ally Yussuf ‘Tigana’ na wengineo kabla ya kuhamia Sigara na baadaye Simba SC kisha kumalizia soka yake Kajumulo.   
Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu. Amin

Post a Comment

Previous Post Next Post