NEWS: AMRI KIEMBA ASAINI SIMBA KWA MILLIONI 35


Hatimaye mazungumzo baina ya Klabu ya Simba na mchezaji Amri Kiemba yamemalizika kwa pande hizo mbili kukubaliana kuongeza mkataba mpya.

Mchana wa leo Simba ilikuwa kwenye jitihada nzito kuhakikisha inamzuia Kiemba kusaini Yanga kwa kumpa ofa nono ya mkataba mpya, Kiemba alikuwa akihitaji kiasi cha millioni 38 ili asaini msimbazi lakini baada ya mazungumzo marefu Kiemba amekubali kusaini kwa kiasi cha millioni 35 kwa miaka miwili.

Pia Kiemba atakuwa analipwa mshahara wa millioni 2 kwa mwezi. Alisaini mkataba huo mbele ya kaimu makamu mwenyekiti  Mzee Kinesi.

Post a Comment

Previous Post Next Post