OMBI LA DARK MASTER KWA JK, NGWEA ALIKUWA ANAITWA MTOTO WA JAKAYA....

Ombi la Dark Master kwa Rais Kikwete, “Ngwea alikua anaitwa mtoto wa Jakaya..tufikirie wana Chemba tusife masikini”

Member wa kundi la Chemba Squared ambalo ni kundi lililomjumuisha marehemu Albert Mangwea, Mez B wa Area C, na Noorah a.k.a baba Star amepaza sauti yake akiwa jijini Mwanza alipopewa nafasi ya kuzungumzia jinsi alivyopokea habari za kifo cha msanii mwenzake (Ngwea) na ameliweka hewani ombi lake kwa mheshimiwa rais Jakaya Kikwete.

Akizungumza katika kipindi cha Amplifaya cha Clouds Fm, Mwana chamber ametumia fursa hiyo kumuomba rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mh. Jakaya Mrisho Kikwete kuwakumbuka wasanii ili wasife masikini kwa kuwa wanakutana na changamoto nyingi. Amesema marehemu Ngwea alikuwa anaitwa mtoto wa Jakaya na kwamba walipiga kampeni sana kumuweka bwana mkubwa juu, ila alionesha mshangao kuona sasa Ngwea anachangishiwa pesa ya kumrudisha Tanzania, na kumuomba bwana mkubwa kuingilia.

Dark Masters amemuomba mheshimiwa rais aingilie kati na awaangalie pia wanachemba wasife masikini, “tufikirie wana chemba tusife masikini.”

Pia ameelezea jinsi alivyopokea taarifa za msiba za msanii mwenzake kwa masikitiko, na katika hali ambayo hakuitegemea lakini anasema mwisho ilimbidi aamini kwa kuwa hiyo ni njia yetu wote.

Mwili wa Marehemu albert Mangwea aliyefariki huko Johannesburg Afrika kusini unatarajiwa kufika Tanzania jumapili hii saa nane mchana.

Post a Comment

Previous Post Next Post