RADIO ONE YAMFAGILIA DK. ASHA-ROSE MIGIRO KWA KUKIENZI KISWAHILI

Dr. Asha-Rose Migiro


DAR ES SALAAM, Tanzania
NAIBU Katibu Mkuu Mstaafu wa Umnoja wa Mataifa, Dk. Ash-Rose Migiro amesifiwa kwa umahiri wa wake wa kutoingiza athari za kiingereza katika kiswahili, anapozungumza au kuhutubia, licha ya kuishi na kufanya kazi nje ya Tanzania kwa miaka mingi.

Amesifiwa kwamba amekuwa akizungumza kiswahili fasaha kisichochanganywa na kiingereza, kwa athari za maneno au utamkaji kwenye mikutano ya hadhara au katika mazungunzo ya kawaida na watu.

Sifa hizo zimetolewa leo na Mtaalam wa Kiswahili kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Mussa Kaoneka, katika kipindi cha lugha ya Kiswahili, kilichokuwa kikitangazwa na Kituo cha Radio One kilichopo Mikocheni, Dar es Salaam.

"Hizi athari zinatokana na watu wengi kupenda kutukuza mno lugha za wenzetu, na tatizo limekuwa likidhaniwa kwamba huenda ni kitokana na mtu kuwa ughaibuni kwa mda mrefu, lakini mbona wapo baadhi ya Watanzania ambao wamekaa na kufanya kazi kwa muda mrefu nje, lakini wakizungumza Kiswahili utasuuzika moyo kwa jinsi wanavyokienzi wanapoongea", alisema Kaoneka na kuongeza;

"Mmoja wa Watanzania hawa naomba  nimtaje, ni Dk. Asha-Rose Migiro aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, huyu ukimkuta anazungumza kwenye mikutano ya hadhara hata kwa kutumia hotuba ambayo hakuiandika, huwezi kumsikia amechanganya hata neno moja la kiingereza katika mazungmzo yake au kuzungumza kwa haiba ya kizungu.

Kaoneka alisema, mbali ya hotuba, hata katika mazungumzo ya kawaida Dk. Asha-Rose ambaye kwa sasa ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, akiamua kuzungumza kiswahili ni kiswahili fasaha kisicho na mchanganyiko wa neno la Kiinereza hata moja.

Katika kipindi hicho kilichorushwa kuanzia saa mbili asubuhi, kikiongozwa na mtangazaji Lugendo Madege, walikuwa wanajadili athari mbaya na nzuri za lugha nyingine kwenye Kiswahili katika zama hizi za utandawazi.

Walisema, athari nzuri ni pamoja na Kiswahili kuweza kupata maneno mapya hasa ya majina ya vitu na teknbolojia ambavyo kabla ya udandawazi havikuwepo Tanzania na hivyo kulikuwa hakuna majina rasmi ya kuvitaja na athari mbaya ni baadhi ya watu kuchukua maneno ya Kiingereza na kuyapa tafsiri  ya 'sisisi' ambayo yanakiharibu Kiswahili.

Kaoneka aliyataja baadhi ya maneno yanayotokana na tafsiri za aina hiyo kuwa ni 'Mwisho wa siku' linalotokana na neno la Kiingereza 'at the end of the day' ambalo kwa mujibu wa mtaalam huyo tafsiri yake sahihi ni 'hatimaye', na mtu kusema "siku hizi nafanyakazi na Benki, wakati usahihi ni "nafanyakazi benki".

Alifafanua kuwa kusema, "nafanyakazi na Benki" ikimaanisha kuajiriwa Benki, siyo sahihi, kwa kuwa kutamka hivyo kuna maanisha kwamba mhusika na benki wanafanya kazi pamoja. IMEYATARISHWA NA BASHIR NKOROMO

Post a Comment

Previous Post Next Post