Wachezaji wawili wa kandanda wa timu ya taifa ya Ufaransa Franck Ribery na Karim Benzema wameshtakiwa mahakamani leo mjini Paris kwa kutoa malipo ili kushiriki ngono na kahaba mwenye umri mdogo.
Mshambuliaji wa Bayern Munich Ribery na mwenzake wa Real Madrid Karim Benzema wanakabiliwa na adhabu ya hadi miaka mitatu gerezani na faini ya juu ya kiasi cha euro 45,000 kama watapatikana na hatia ya uhalifu huo.
Wachezaji hao wote wawili wamekanusha mashtaka na msichana aliyehusika Zahia Dehar, ametoa ushahidi kuwa wanasoka hao wawili hawakujua kuwa alikuwa na umri wa chini ya miaka 18 wakati walipofanya naye kitendo cha ngono mwaka wa 2008 na 2009.
Japokuwa umri unaoruhusiwa kisheria nchini Ufaransa wa mtu kuwa na ufahamu ni miaka 15, kumlipa yeyote mwenye umri wa chini ya miaka 18, ili kushiriki naye ngono ni uhalifu.
Ribery mwenye umri wa miaka 30, alikiri kufanya mapenzi na Dehar, lakini anasisitiza kuwa hakujua kuwa alikuwa na umri mdogo.
Benzema naye amekanusha kabisa kufanya kitendo hicho
Post a Comment