Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi (T).
--
Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP
Said Mwema, amefanya mabadiliko ya makamanda na wakuu wa upelelezi
katika baadhi ya mikoa hapa nchini.
Katika mabadiliko hayo aliyekuwa
Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Michael
Kamhanda amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi na nafasi yake inachukuliwa
na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ramadhani Mungi ambae alikuwa
Makao Makuu ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai.
Aidha, DCP Ally Mlege aliyekuwa
Makao Makuu ya Polisi amehamishiwa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwenda
kuwa Mkuu wa utawala na raslimali watu.
Vilevile, Kamanda wa Polisi mkoa
wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela amehamishiwa Makao Makuu ya
Upelelezi wa makosa ya jinai na nafasi yake inachukuliwa na aliyekuwa
Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Arusha ACP Camilius
Wambura. Aidha, ACP Duwan Nyanda aliyekuwa Makao Makuu ya Upelelezi
anaenda kuwa Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa wa Arusha.
Uhamisho huo ni wakawaida kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi.
Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi (T).
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi (T).
Post a Comment