TRA YAKIFUNGA KIWANDA CHA SAMAKI KWA SABABU YA KODI!!




  • Akizungumza baada ya kukifungia kiwanda hicho, Ofisa Kodi wa TRA kutoka Dar es Salaam, Toans Silvanus alisema kiwanda hicho kimeshindwa kulipa deni hilo la mwaka mmoja.
Musoma. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imekifungia Kiwanda cha Kusindika Minofu ya Samaki cha Prime Catch (Export) Ltd, baada ya kushindwa kulipa mapato ya Sh1.1 bilioni. Akizungumza baada ya kukifungia kiwanda hicho, Ofisa Kodi wa TRA kutoka Dar es Salaam, Toans Silvanus alisema kiwanda hicho kimeshindwa kulipa deni hilo la mwaka mmoja. “Kiwanda hiki kimekuwa kikikumbushwa kulipa mapato mara kwa mara, barua wamekuwa wakiandikiwa kuhusu umuhimu wa kulipa mapato bila shuruti, lakini wameshindwa,” alisema. (Florence Focus).

Post a Comment

Previous Post Next Post