Uchaguzi mdogo wa madiwani Arusha waahirishwa


Imearifiwa kuwa Tume ya taifa ya Uchaguzi imesimamisha kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata nne jijini Arusha.

Kwa mujibu wa msimamizi mmoja wa kituo cha uchaguzi mkoani Arusha na kwa mujibu wa mazungumzo kwa njia ya simu na Radio TBC FM kutoka Zanzibar, Jaji mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Damian Lubuva ambaye ni mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi amesema uchaguzi huo umeahirishwa kutokana na uwezekano wa wapiga kura kutoshiriki kikamilifu katika zoezi la kupiga kura kwa sababu ya hofu na wengine wakiendelea na shughuli za mazishi ya waliofariki katika mlipuko wa bomu uliotokea hapo jana jioni:

“Tume imeahirisha uchaguzi katika kata nne za Arusha mjini kutokana na tukio hilo ambalo linawapa Wananchi hofu wakati wa kupiga kura hivyo uchaguzi umeahirishwa hadi tarehe 30 Juni...”  

“...jioni ya Juni 15, 2013 tulipata taarifa ya tukio kule Arusha ambako uchaguzi unafanyika katika kata nne za pale mjini, katika kata moja wapo ya kumalizia kampeni za mwisho bomu likatupwa na watu kufariki pamoja na wengine kuumia, kutokana na hilo tumeona siyo wakati muafaka kwa uchaguzi kuendelea kwa sababu wengine wanaendelea na shughuli za mazishi,” alisema Jaji Lubuva.

Post a Comment

Previous Post Next Post