Serikali ya Uingereza huenda ikaomba msamaha na kuandaa fidia kwa waliokuwa wanachama wa harakati za ukombozi wa Kenya Mau Mau.
Waliokuwa
wanachama wa kundi hilo waliwasilisha kesi mahakamani kwa mateso na
dhuluma waliodai kutendewa na uliokuwa utawala wa ukoloni miaka ya 50.
Mwezi
Oktoba mwaka 1952 ukoloni wa Uingereza nchini Kenya ulitangaza hali ya
hatari na kuanzisha harakati za kijeshi zilizolenga vuguvugu la Mau Mau.
Kundi hilo lilikabiliana vikali na majeshi ya Uingereza likipinga kunyang’anywa ardhi na kutaka uhuru wa kujitawala.
Miongo
kadhaa baadae wanachama wa kundi hilo walionusurika wamekuwa na vita
vingine ambapo walifika katika mahakama ya London na kuwasilisha madai
wakitaka Uingereza iwaombe radhi na kuwafidia kwa dhuluma walizotendewa.
Wakati
huo huo leo jijini Nairobi nchini Kenya linafanyika kongamano la
kitaifa linalohusu jinsi ya kuhamasisha jamii umiliki na matumizi ya
ardhi.
Kongamano hilo linaongozwa na muungano wa kutetea masuala ya umiliki wa ardhi nchini humo National Lands Alliance.
Post a Comment