WANAFUNZI WALIOSOMA SHULE ZA KATA VYUO VIKUU WAMTAKA LOWASSA AWANIE URAIS 2015



Mbunge wa Monduli, ambaye pia ni waziri mkuu mstaafu, Edward Lowasa, akisalimiana na wanafunzi wa chuo kikuu cha UDOM waliotoka shule za sekondari za kata, wakati walipofika nyumbani kwake mkoani Dodoma kutoa shukrani zao kwa hatua waliyofikia kielimu
Hamida Salum mwanafunzi wa mwaka wa kwanza UDOM, akizungumza kwenye hafla hiyo Juni 25, 2013
Mh. Lowasa katikati, Dkt. Mahanga (Kulia) na Parseko Korne wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi hao.
 
Na Father Kidevu Blog, Dodoma
Wanafunzi wa Chuo Kikuu ch DODOMA, maarufu kama UDOM, ambao walifika hapo wakitokea zile shule za makabwela (Shule za Kata), wamemtaka Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowasa, achukue fomu za kugombea urais 2015 muda utakapowadia.
 
Pia wameahidi kujichangisha fedha kwa ajili ya malipo ya fomu hizo endapo italazimika.

Kauli hiyo ya kwanza kutoka kwa makundi na watu wasiokuwemo ndani ya siasa, ilitolewa Jumatatu usiku nyumbani kwa Lowasa mjini Dodoma, wakati kundi nla wanafunzi hao walipofika kutoa shukrani zao kwa hatua waliyofikia ikiwa ni matunda ya shule hizo, ambazo muasisi wake ni mbunge huyo wa Monduli.
 
“Mimi ninayofuraha kusimama hapa leo hii, nikiwa mtu tofauti, kwa maana ninayesoma elimu ya juu, baada ya kufanikiwa ,kuendelea na elimu ya sekondari kupitia shule za kata pale Kiluvya Dar es Salaam” anasema Hamida Salum ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza hapo UDOM.
 
“Wewe ni jembe, kama uliweza kusimamia ujenzi wa shule za kata kwa kipindi kifupi cha miaka 2, ninahakika unaweza kufanya men gi zaidi endapo utakuwa rais wan chi hii” mwanafunzi mwingine wa mwaka wa kwanza, Clementina Ophoro alisema, kwenye salamu za mwanafunzi mmoja mmoja wakati wa utoaji shukrani kwa Lowasa.
 
Lowasa wakati akiwa waziri mkuu wa Tanzania, kwenye mwanzoni mwa awamu ya n ne ya utawala wa rais Jakaya Kikwete, aliweza kusimamia ujenzi wa shule za kata kote nchini, ili kutoa nafasi zaidi za wanafunzi wa makabwela, walioishindwa kendelea na masomo kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na uhaba wa madarasa.

Kwa sasa shule hizo zimekuwa zikibezwa na watu mbalimbali kwa maelezo kuwa hazina walimu wa kutosha na uhaba wa vifaa vya kufundishia ikiwemo vyumba vya maabara.
 
“Mimi ninawashangaa watu wanaosema kuwa eti shule za kata hazifai, kwa vile hazina walimu na vifaa. Haya maneno ni ya kupuuzwa, kwani binadamu hupaswi kukwepa changamoto za maisha” alisema mwanafunzi mwingine Victor Mafuru pia wa mwaka wa kwanza.
 
Wanafunzi hao wa UDOM waliotoka kwenye shule za sekondari za kata, wameamua kuanzisha umoja wao kote nchini, ili kuendeleza ndoto za kuhakikisha kila mwanafunzi wa mtu masikini anapata elimu.
 
Kwa kuanzia wanafunzi hao wapatao 600, wameahidi kufundisha bure kwenye shule za umma, wawapo likizo baadaye mwishoni mwa mwezi huu wa Juni.
 
Kwa upande wake, Lowasa ambaye alikuwa pamoja na naibu waziri wa kazi na ajira, Dkt. Makongoro Mahanga, mbunge wa Kigoma mjini, Peter Serukamba, na mkuu wa mkoa wa Singida, Parseko Kone, aliwapongeza wanafunzi hao kwa moyo wao wa shukrani na kuwataka wasikatishwe tama na maneno yanayotolewa juu ya ubora wa shule hizo, kwani yeye binafsi anajivunia juhudi zake kupitia sera za chama cha Mapinduzi, zimeweza an galau kutoa wanafunzi wengi kutoka shule hizo kujiunga na vyuo vikuu.

Post a Comment

Previous Post Next Post