WATU WAWILI WALIOKUWA NA BASTOLA KATIKA PIKIPIKI WATIWA MBARONI NA POLISI JIJINI DAR LEO



Askari kanzu (kulia) akiwa ameshika bastola aliyokutwa nayo mtu mmoja aliyekuwa amepakiwa katika pikipiki aina ya Boxer yenye namba za usaji T 961 CJW katika mtaa wa Makunganya jirani kabisa na benki ya Posta jijini Dar es Salaam mchana huu. Kutokana na kuongezeka kwa matukio ya ujambazi wa kutumia pikipiki Polisi wameimarisha ulinzi na hasa katika maeneo ya mabenki. Picha Na:-  othmanmichuzi.blogspot.com
Asklari kanzu akiwa na bastola alikamatwa nayo mtu mmoja aliyekuwa amepakiwa katika pikipiki aina ya Boxer.
 Watu waliokamatwa wakijaribu kuwasiliana na ndugu zao.
 Pikipiki waliyokuwa wakitumia. 
 Ofisa wa Polisi akijaribu bastola waliyokutwa nayo watu wawiliwaliokuwa katika Pikipiki Posta Mpya jirani na Benki ya Bosta leo.
 Ngoja niijaribu.
 Heee ina risasi!
 Ofisa wa Polisi aliyeefika katika eneo la tukio akiendelea kuikagua.
 Mtu aliyekutwa  na bastola hiyo, ambaye alijitambulisha kama mfanyabiashara.
 Polisi wakifanya mawasiliano na wenzao wa doria kuomba msaada wa gari.
 Mtuhumiwa aliyekutwa na bastola akihojiwa.
 Akiwasiliana na ndugu zake.
 Akichukuliwa maelezo na Ofisa wa Polisi.
 Dereva wa Pikipiki naye akichukuliwa maelezo yake.
 Unaitwa nani, unaishi wapi, unafanya kazi gani, kabila gani, Ofisa wa Polisi akimuhoji mtuhumiwa.
 Ofisa wa Polisi akiwasha pikipiki kwa ajili ya kuondoka na watuhumiwa kwenda Kituo cha Kati.

Post a Comment

Previous Post Next Post