Hitmaker
wa Samson na Delilah, Timbulo ambaye yupo mbioni kuachia video ya ‘Sina
Makosa’ wiki ijayo, amesema yeye ni mwanachama mkubwa wa kambi ya
MwanaFA kwakuwa bado yupo yupo sana. Amesema hana mpango tena wa kuoa na
isahaulike kabisa baada ya kuona kuwa wanawake wengi wanampenda kwakuwa
ni msanii na hawana mapenzi ya dhati.
Timbulo amesema hayo baada ya kuwaahidi mashabiki wake kwamba
anakaribia kuoa ila kwa sasa amebadilisha mawazo baada ya uhusiano wake
kumwendea ndivyo sivyo na kumkata mudi na matarajio ya kufunga ndoa.
Ameiambia Hisia za Mwananchi kuwa msichana aliyekuwa amepanga amfanye mke amemzingua vibaya.
“Sahau kuhusu mimi kuoa, muolewaji hakuna bana, kwa wastani wa maisha
ya furaha ya siku 1 kwa sita, zilizobaki kwenye week ni ugomvi, huzuni
na kutoelewana siwezi, nitakufa na pressure,” amesema.

Post a Comment