Majaji
wa Epiq Bongo Star Search Master J, Salama Jabir na Chief Judge Madam
Ritha Paulsen wakifurahi jambo wakati wa usaili wa vijana wa Dar es
Salaam uliofanyika uwanja wa Taifa.
Wasichana
hawa ni mapacha ambao walijitokeza kwenye usaili wa shindano la Epiq
Bongo Star Search (EBSS) uliofanyika kwenye uwanja wa taifa Dar es
salaam, walilazimika kuimba pamoja na ni tukio la kwanza kwa washiriki
wawili kuimba pamoja kwenye usaili wa mwaka huu.
Wasichana
hawa mapacha waliojitokeza kwenye ushiriki wa shindano la EBSS 2013
mkoani Dar es salaam wakisikiliza jambo kutoka kwa Jaji Mkuu wa EBSS
Ritha Paulsen.
Mwanafunzi
wa kidato cha nne katika sekondari ya Yusuph Makamba, Dar es salaam
akifurahi baada ya kupita awamu ya kwanza ya shindano la EBBS 2013.
Umati wa vijana wakisubiri kufanyiwa usaili.
Umati wa vijana uliojitokeza kwenye usaili wa EBSS 2013 kwenye uwanja wa taifa.
Mtangazaji
wa Clouds Radio Millard Ayo ambaye naye alishiriki katika kutoa maamuzi
kwenye usaili huo akishow love na Majaji w EBSS mara baada ya kumaliza
zoezi la usaili jijini Dar kwenye Uwanja wa Taifa.
Shindano
la kuimba la Epiq BSS limemaliza usaili wake ambao kwa mwaka huu
umefanyika katika mikoa sita ya Arusha, Mbeya, Mwanza, Zanzibar, Dodoma
na kumalizia Dar es Salaam.
Usaili
wa Dar es Salaam uliofanyika mwishoni mwa wiki hii ndio umehitimisha
zoezi la kusaka vipaji, huku mwishoni mwa wiki hii washiriki wakijiandaa
kuingia kambini kwa ajili ya mchujo wa kwanza.
Wiki
hii washiirki waliopatikana mikoani wataungana na washiriki wa hapa Dar
es salaam katika mchujo wa awali wa kupata washiriki watakaoingia
katika kambi rasmi ya EBSS 2013.
Kwa
mkoa wa Dar es salaam washiriki waliopatikana ni 20 huku mikoa mingine
ya Arusha, Mwanza, Dodoma, Mbeya na Zanzibar washiriki waliopatikana ni
sita kila mkoa hivyo kufanya jumla wa washiriki watakaoingia katika
mchujo wa awali kuwa 50.
Shindano
hilo ambalo mwaka huu lilikuwa na utaratibu mpya wa kutumia majaji
wenyeji kutoka katika kila mkoa, ambapo kwa upande wa Mbeya kulikuwa na
majaji ambao ni watangazaji wa radio huku usaili wa Dar es Salaam
ukichagizwa na mchezaji wa mchezo wa mpira wa kikapu wa ligi ya
Marekani (NBA) Hashim Thabeet aliyekuwa kama jaji mwalikwa.
Akizungumza na baadhi ya wahiriki waliojitokeza Hashim aliwataka vijana kutokata tamaa katika kutafuta mafanikio kupitia muziki.
Alisema
kuwa anaamini Tanzania kuna vipaji vingi vya muziki ambavyo vinatakiwa
kuendelezwa kufikia viwnago vya kimataifa, lakini ili kufanikisha hilo
inatakiwa vijana wenyewe kujiamini na kuongeza nia ya kweli katika
kutafuta kung’arisha nyota zao.
Aliwataka
kutambua kuwa nidhamu na kujituma ndio siri kubwa ya mafanikio katika
sanaa na kazi yoyote ile na hivyo aliwasihi kujitambua na kutafuta
mfanikio hayo.
Akizungumzia
shindano hilo kwa mwaka huu, jaji mkuu wa shindano hilo, Ritha Paulsen
alisema mchuano utakuwa mkali hasa kutokana na kuchagua washiriki
wakali kutoka kila mkoa.
‘Mwaka
huu ushindani utakua mkali kuliko mwaka jana, lakini pia kutakuwa na
burudani zaidi kutoka kwa washiriki kama ambavyo imezoeleka’ alisema
Ritha.
Naye
Afisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan alisema Zantel imezidi
kuboresha shindano hilo, huku akiwataka watanzania watarajie makubwa
zaidi mwaka huu katika kuzalisha vipaji na pia kupata burudani kubwa.
‘Tutatoa
zawadi kadha wa kadha shindano litakapoanza, lakini pia wale ambao bado
wanataka kushriki wanaweza kutumia njia ya simu kufanya usaili wao’
alisisitiza Khan.
Washiriki
wanaotaka kufanya usaili kwa njia ya simu wanapaswa kupiga namba
0901551000 au watume ujumbe mfupi kwenda 15530 kupata maelezo ya namna
ya kujiunga.
Post a Comment