Vijana wa Youth Power Group wakiwa na Bango lao linalohamasisha vijana
kupinga matumizi ya madawa ya kulevya kwenye Barabara ya Obama.
Mchungaji Marcos Braga wa Kanisa la Universal la Ufalme wa Mungu akijumuika kwenye zoezi hilo na vijana wake.
Viongozi, walinzi shirikishi na baadhi ya wananchi wa kata ya Kivukoni
katika manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam wakishirikiana na waumini
takriban 100 wa kanisa la Uokovu na Ufufuo la Kidongo Chekundu leo
wameendesha zoezi la kufanya usafi kwa kuokota takataka na kufagia
kuanzia eneo la ufukwe wa Ocean Road hadi eneo la Aga Khan sambamba na
kampuni ya usafi katika manispaa hiyo ya Green Waste pro Ltd.
Akizungumza na vyombo vya habari Mtendaji wa kata ya Kivukoni Bw. Renatus Ruhungu amesema kwa leo wanashirikiana na wenzao wa Universal Church wa kata ya Gerezani na wadau wengine pamoja na Kampuni ya Green Waste Pro lakini wakati mwingine watashirikisha wadau wengine katika utaratibu wao wa kufanya

usafi kila wiki ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya waraka wa Mkurugenzi na mkuu wa Mkoa.
Ameongeza kuwa wameona wakifanya wao tu ile dhana ya kuwa usafi ni wa kila mtu watakuwa wameipoteza, hivyo wakaona ni vyema sasa kushirikisha taasisi na jamii zilizo kwao na mbazo ziko nje pia kuzialika kuja kushikiana na wao kufanya usafi ili wananchi waone kumbe sio kazi ya serikali.
Naye wa Kiongozi wa kanisa la Universal la Ufalme wa Mungu Mchungaji Marcos Braga amesema wao kama kanisa wakiangalia nchi wanaona vitu vipi vinatakiwa kuendelezwa na nini kinatakiwa kifanyike, hivyo wameamua kutoka nje kwenda kuendeleza mji wao kwa kuanzia na usafi.
Amefafanua kuwa kikundi cha vijana wa kanisa hilo kinashiriki katika shughuli mbalimbali ambazo zinaigusa jamii moja kwa moja na pia tuna kampeni inayosema ‘Kijana Mwerevu Sema hapana kwa Madawa ya Kulevya’ kwa kuwa vijana wengi wanaangukia katika matumizi ya dawa hizo na kufanya maendeleo ya taifa la kesho kuwa duni.

Mtendaji wa kata ya Kivukoni Bw. Renatus Ruhungu akizungumzia hatua yao
ya kushirikisha wadau katika zoezi la kufanya usafi manispaa ya Ilala,
ambapo amesema mwezi ujao wanajiandaa kushirikiana na wenzao wa Chuo cha
IFM, ili vijana hao waweze kuhamasika na suala la usafi na kuwa
wataendelea kushirikisha taasisi, vikundi na asasi mbalimbali ili
zifahamu kuwa usafi ni jukumu la kila mtu bila kuisahau kampuni ya usafi
ilala ya Green Waste Pro ltd. Katika zoezi hilo leo wameshirikiana na
Kikundi cha vijana cha Youth Power Group cha Kanisa la Universal la
Ufalme wa Mungu kusafisha fukwe ya Bahari ya Hindi kuanzia eneo la Ocean
Road Hospital mpaka Aga Khan.
Mchungaji wa Kanisa la Universal la Ufalme wa Mungu Marcos Braga
akizungumza wakati wa zoezi la pamoja na viongozi wa kata ya Kivukoni na
Kampuni ya Green Waste Pro kufanya usafi kutoka ufukwe wa Ocean Road
hadi eneo la Aga Khan ambapo amesema ni jukumu lao kuendeleza maisha ya
baadae ya taifa letu, hivyo kila wakati wanajitoa kushiriki miradi na
kazi tofauti zitakazofanikisha kulikomboa taifa kimaendeleo likiwemo
suala la usafi wa jiji.
Ameongeza kuwa walichifanya leo sio mwishi bali watakuwa wakifanya mara
mbili kwa mwezi katika maeneo tofauti hivyo ameomba ushirikiano kwa
serikali na wadau mbalimbali.
Mchungaji Marcos Braga wa Kanisa la Universal la Ufalme wa Mungu
akisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi ya Kata ya Kivukoni kabla
kuelekea eneo la tukio kwa ajili ya kushiriki zoezi la kusafisha fukwe
ya Bahari ya Hindi kuanzisha Ocean Road Hospital mpaka Aga Khan.
Mtendaji wa Kata ya Kivukoni Renatus Ruhungu (aliyeketi) Afisa Usafi wa
Manispaa ya Ilala Bw. Samuel Bubegwa (na wa tatu kushoto), Meneja
Msaidizi wa Kampuni ya Usafi ya Green Waste Pro ltd Bw. Abdallah Mbena
(kushoto) katika picha ya pamoja na baadhi ya vijana wa kikundi cha
Youth Power Group cha Kanisa la Universal la Ufalme wa Mungu.
Wanakikundi cha Youth Power Group wa Kanisa la Universal la Ufalme wa
Mungu wakielekea kwenye fukwe za bahari ya Hindi kwa ajili ya zoezi la
usafi.
Picha juu na chini ni Mtendaji wa Kata ya Kivukoni Renatus Ruhungu
(mwenye kofia nyeusi) akishiriki zoezi hilo na baadhi ya wanakikundi.
Bw. Said Mazingira wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd. akishiriki zoezi
hilo na Kikundi cha Youth Power Group kutoka kata ya Gerezani.
Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Usafi ya Green Waste Pro Ltd
akishirkiana na vijana wa Kanisa la Universal La Ufalme wa Mungu wakati
wa zoezi hilo.
Kazi imepamba moto.
Post a Comment