Taarifa kutoka katika magazeti ya leo;
"Wanawake
wawili raia wa Tanzania wametambuliwa kuwa ndiyo wanaodaiwa kuingiza
shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8
nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.
Akizungumza
na NIPASHE jana, Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na
Dawa za Kulevya, Geofrey Nzoa, alisema haijafahamika wanawake hao
wanatoka mikoa gani.
Kamanda
Nzoa aliwataja wanawake hao kuwa ni Agnes Jerald ambaye alisema
hajapiga hesabu ya umri wao, ila alizaliwa mwaka 1988 kwa maana hiyo ana
umri wa miaka 25 na Melisa Edward ambaye alisema amezaliwa mwaka 1989
kwa maana hiyo atakuwa na umri wa miaka 24. Wawili hao bado wanaendelea
kuhojiwa na polisi wa Afrika Kusini".
Mwanadada
Agnes Masogange kwa sehemu kubwa anahisiwa kuwa ndiye mhusika ambaye
yupo kizuizini huko Afrika kusini kwa kesi hii, bado tunaendelea
kufuatilia kwa makini ili kupata uthibitisho wa taarifa hizi na kama ni
kweli Mtuhumiwa aliye kamatwa ni Agnes Jerald... maarufu zaidi kama
Agnes Masogange.
Aina
yake ya maisha ya hali ya juu bila jamii kujua wazi ni kitu gani
anachokifanya kujipatia kipato, pamoja na binti huyu kuwa na Safari
nyingi za Afrika Kusini ni moja ya sababu ambazo zinaongezea nguvu swala
la kuwepo kwa ukweli katika taarifa hizi kwa mujibu wa wadau.

Post a Comment